Kampuni ya Huawei mbioni kuutambulisha mpango wake wa utoaji elimu kwa njia ya Tehama

Kampuni ya Huawei, yenye makao yake makuu mjini Shenzhen nchini China, inatarajia kuutambulisha mpango wake wa utoaji elimu kwa njia ya Tehama, unaojulikana kwa jina la E-education.

Hayo yalibainishwa mapema wiki hii na maofisa kuytoka kampuni hiyo wakati wa ziara ya waandishi wa habari nchini China waliotembelea kujionea namna mradi ‘Smart education’ wanaoutekeleza katika shule ya msingi Baogang nchini China na kuwa wa mafanikio.

Meneja Mahusiano wa kampuni hiyo, Schloss glenn James, alisema kuwa kuanzishwa kwa mradi kama huo wa elimu kwa njia ya teknolojia ya Tehama kwa shule za msingi na sekondari itasaidia kuinua kiwango cha elimu nchini kama ilivyothibitika katika mradi ulioanzishwa katika shule ya msingi Baogang.

James alisema Huawei kwa sasa wamejikita zaidi katika miradi ya mifumo ya elimu kwa mtandao ambapo kupitia mradi huu, matarajio ni kuboresha kiwango cha elimu kwa kiwango cha juu kupitia teknolojia ya Tehama kwa ajili ya kufundishia na kusoma.

Kwa mazingira hayo, Huawei wamekuwa wakihamisha ujuzi wao kwenda kwa watumishi mbalimbali nchini kwa kuwatumia wataalamu waliobebea ndani ya Huawei.

Meneja huyo alisema katika kutekeleza jukumu hilo, Huawei ikiwa na watumishi 120, wamekuwa wakitoa mafunzo na elimu kwa vitendo kwa wanafuzni wa fani ya Tehama.

Sambamba na hayo, mkakati wa kampuni hiyo ya Huawei, ni kupanua wigo wao katika uboreshaji wa miundombinu ya ICT kwa lengo la kuiunganisha nchi ya Tanzania.

Alifafanua kwamba ajenda ya kampuni hiyo ni kuhakikisha wanaendelea kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi wa kiwango cha kimataifa katika kuyafikia mageuzi ya kweli katika nyanja mbalimbali kupitia utaalamu wa teknolojia ya tehama.

Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari Tanzania, wakiwa katika picha ya pamoja mjini Shenzhen, China, walipokwenda kutembelea makao makuu kampuni ya Huawei na kuijionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni hiyo ikwemo utekelezaji wa mradi wa elimu wa Smart Education

Kwa mwaka huu, Huawei wamekuwa katika mkakati kamambe wa kutafuta njia mbadala na bora zaidi za kuisaidia Serikali katika malengo yake yake ya kiuchumi ifikapo mwaka 2020/2025.

Huawei wamekuwa wakifanya hivyo kwa maslahi ya nchi katika kutimiza wajibu wao wa kuhakikisha vyanzo na njia mpya za kuharakisha maendeleo zinapatikana.

About Zanzibar Daima 1611 Articles
Zanzibar Daima, Jana, Leo na Kesho

Be the first to comment

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.