Kafulila na siri za kuhama vyama miezi ya Novemba na Disemba

Nilitokea kuvutiwa sana na aliyekuwa mbunge wa Kigoma Kusini kwa chama cha NCCR-Mageuzi, David Kafulila. Hali hii ilinivutia zaidi pale mwezi Mei 2014 alipoibuwa mjadala wa uliopewa jina la “Sakata la Esrow”, sakata hili ndilo lililomsababishia Kafulila mambo mengi sana yakiwemo mazuri na mabaya.

Sakata la Escrow ilikuwa ni tuhuma kubwa mno ya wizi wa mabilioni ya mapesa ambayo yalichotwa na viongozi wa serikali ya Jamuhuri ya Tanzania kinyume na sheria na kwa kitendo hicho cha Kafulila kuibuwa uovu huo ilimsababishia kutengeneza maadui wengi sana, sambamba na kupokea vitisho na hadi kufikia kufananishwa na mnyama tumbili, lakini kwa upande mwengine pia Kafulila alipata heshima kwa Watanzania wengi na kuthibitisha hilo ndipo Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR Mageuzi), David Kafulila alikabidhiwa Tuzo ya utetezi wa haki za binadamu na Utawala Bora ya mwaka 2014.

Na Ali Mohammed

Mbali ya tunzo hio, katika mwezi wa Julai mwaka huu huu Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli alimsifu Kafulila wakati alipotembelea na kuwahutubia wakazi wa Kata ya Nguruka katika hafla ya uzinduzi wa mradi mkubwa wa maji uliopo Tarafa ya Nguruka katika Wilayani Uvinza. “Wakamtisha wengine kumpeleka mahakamani, wakamtukana wee, wengine wakamuita tumbili, sasa tumbili amefanya makubwa kwa ajili ya Watanzania. Wao ndio matumbili, huyu (Kafulila) alifanya kazi ya Mungu ya kuwatumikia Watanzana,” alisema Rais Magufuli.

Nilianza na maelezo hayo kidogo ili nikusogeze karibu wewe msomaji asiyemjuwa David Kafulila aambaye hivi majuzi Disemba 22 alifanya maamuzi yake ya kikatiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Chadema, lakini ikumbukwe kwamba David Kafulila hii si mara yake ya kwanza kutangaza kuhama na kuhamia chama au kufukuzwa chama, kumbukumbu zangu zinanithibitishia kwamba hii ni mara ya nne kwa David Kafulila kupitia katika hatua aidha iwe kuhama, kuhamia au kufukuzwa.

Lakini ninapta masuali juu ya Kafulila kwa sababu mambo yote hayo yanayotokea Kafulila basi huwa yanatokea mwisho wa mwaka, aidha huwa ni mwezi wa Novemba au Disemba na haijawahi kutokea mwanzoni mwa mwaka au kati kati ya mwaka, na hapa nitakuonyesha:

  • Novemba 10, 2009 David Kafulila alijivua uanachama Chadema na kuhamia NCCR –Mageuzi, baada ya kuondolewa kwenye nafasi ya Ofisa Habari aliyokuwanayo. Huko Kafulila mwaka 2010 aliingia katika kinyang’anyiro cha kugombania ubunge wa Kigoma Kusini na kafanikiwa kushinda ubunge wa jimbo hilo.
  • Tarehe 18 Desemaba 2011, chama cha NCCR-Mageuzi kilimfukuza uanachama Kafulila na wajumbe wengine sita akiwamo aliyekuwa mgombea urais wa chama hicho katika uchaguzi mkuu wa 2010, Hashim Rungwe, na katika mwezi huo huo Kafulila alikata rufaa na kubaki na ubunge kwa amri ya mahakama. Baadaye alisamehewa na chama chake na kuendelea nacho hadi uchaguzi wa Oktoba 2015 alipogombea tena ubunge na mara hii kuangushwa na mgombea wa CCM.
  • Disemba 16, 2016, mbunge huyo wa zamani wa Kigoma Kusini kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi, David Kafulila, alitangaza kukihama chama hicho na kusema kuwa atajiunga na tena na CHADEMA.
  • Novemba 22, 2017, Kafulila alijivua tena uanachama wa CHADEMA kwa madai kuwa Vyama vya Upinzani haviwezi kuendesha vita dhidi ya ufisadi, ambao ndio ilikuwa ajenda yake kuu.

Sasa hapa ndio najiuliza na kumuuliza Kafulila kwa nini iwe mwisho wa mwaka pekee afanye maamuzi hayo ya kuhama na kuhamia vyama?

About Zanzibar Daima 1611 Articles
Zanzibar Daima, Jana, Leo na Kesho

Be the first to comment

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.