Mzanzibari ateuliwa jopo la majaji Tuzo ya Caine

Na Ahmed Rajab

Ahmed Rajab, mwandishi wa habari wa kimataifa na mchambuzi wa masuala ya kisiasa duniani ambaye ni mzaliwa za Zanzibar, ameteuliwa kuwa mmoja wa majaji wa Tuzo ya Caine kwa Waandishi wa Kiafrika kwa mwaka 2018.

Ahmed Rajab, mwandishi wa kimataifa aliyezaliwa Zanzibar.

Taarifa iliyotolewa na watayarishaji wa Tuzo hiyo ya kimataifa inasema Ahmed Rajab ataungana na majaji wengine wanne, akiwamo Dinaw Mengestu, Mmarekani mwenye asili ya Ethiopia na ambaye mwenyewe ni mwandishi wa riwaya. Dinaw ndiye atakayekuwa mkuu wa jopo hili la majaji.

Akizungumza kufuatia uteuzi huu, Ahmed Rajab amesema ni fahari kubwa kwa nchi yake ya uzawa, Zanzibar.

“Niliona fakhari si ya kwangu mimi binafsi tu, pia ni kwa kule kulikozikwa kitovu changu na kulikonilea mpaka kufika hapa nilipofika,” ameiambia Zanzibar Daima.

Wengine kwenye jopo hilo ni Henrietta Rose-Innes, mwandishi kutoka Afrika Kusini ambaye alishinda tuzo hiyo mwaka 2008; Lola Shoneyin, mkurugenzi wa Tamasha la Ake Arts and Books; na Alain Mabanckou, mwandishi wa kimataifa na profesa wa fasihi katika Chuo Kikuu cha California.

About Zanzibar Daima 1613 Articles
Zanzibar Daima, Jana, Leo na Kesho

1 Comment

  1. Hongera zake na kwa kuipatia umaarufu ZNZ 7 Pemba..

    Ila tunasubiri kwa hamu maoni (article) yako kuhusu kuongeza Mihula ya Urais kwenye Serikali ya Mapinduzi..

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.