Lipumba abwagwa tena kortini

CHAMA cha Wananchi (CUF), upande unaongozwa na Profesa Ibrahim Lipumba kimepata pigo kubwa baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania kupiga marufuku bodi yake kujihusisha na shughuli zozote za chama hicho mpaka shauri la msingi litakapomalizika, anaandika Hamisi Mguta.

Profesa Lipumba, ambaye anatambuliwa na msajili wa vyama siasa nchini, analumbana na Katibu Mkuu wake, Maalim Seif Sharif Hamad, hatua ambayo imesababisha pande hizo mbili kufikishana mahakamani ili kutafuta haki.

Awali, mahakama hiyo iliyatupilia mbali maombi ya Wakili Mashaka Ngole (anayemwakilisha Lipumba) aliyokuwa anaomba Jaji asisome maamuzi hayo kwa madai kuwa Lipumba anakusudia kukata rufaa juu ya maamuzi ya Jaji kukataa kujitoa kusikiliza mashauri ya CUF.

Mahakama Kuu imesema, hakuna hoja za kisheria zinazoizuia kuacha kuendelea na shughuli ilizozipanga.

About Zanzibar Daima 1613 Articles
Zanzibar Daima, Jana, Leo na Kesho

Be the first to comment

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.