Mfumko wa bei juu tena Zanzibar

Kasi ya mfumko wa bei za bidhaa mbali mbali visiwani Zanzibar kwa mwezi wa Disemba imepanda zaidi kwa asilimia 5.9 ukilinganisha na asilimia 5.0 kwa mwezi uliopita wa November 2017.

Mkuu wa kitengo cha Takwimu za bei kutoka ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Khamis Msham alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo huko ofisini kwake Mwanakwerekwe Mjini Unguja ikiwa ni muendelezo wa utoaji taarifa za mfumko wa bei kwa kila mwezi.

Alitaja baadhi ya bidhaa zilizopanda bei kwa mwezi uliopita kuwa ni pamoja na mchele wa Mbeya uliongezeka kwa asilimia 1.2, Mafuta ya kupikia yameongezeka asilimia 0.7, Mchele wa Jasmin asilimia 0.3, Mchele wa Basmati asilimia 0.7, Unga wa Sembe asilimia 1.3 huku Samaki nao wakipanda kwa asilimia  10.1.

Bidhaa nyengine ziliongezeka bei kwa mwezi huo ni mafuta ya vyombo vya moto ikiwamo Mafuta ya Petroli yaliiongezeka kwa asilimia -3.9 Mafuta ya Diesel asilimia 4.7 pamoja na Mafuta ya taa ambayo yaliongezeka kwa asilimia 5.3.

“Lakini pia kwa upande wa vyakula na viwanywaji visivyo kuwa na vilevi navyo imenaokana vimepanda kutoka asilimia 4.2 kwa mwezi ya November hadi kufikia asilimia 6.2 kwa mwezi wa Disember”alisema Msham.

Alisema kuwa kupanda kwa kiwango hicho cha bei za bidhaa mbali mbali kunatokana  na uwepo wa Skuku za krismas pamoja na mwaka mpya hali ambayo ilionekana wananchi wengi kuhitaji huduma za bidhaa hata kwa gharama yoyote.

Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha Uchumi kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BOT) upande wa Zanzibar, Moto Ng’winganele Lugobi alisema kuwa pamoja na upandaji wa bei hizo kuwa ni mkubwa lakini bado haijwa tishio la kupotea kwa bidhaa nchini humu.

Aidha alisema kuwa kwa mujibu wa tathimini yao, hali hiyo ndani ya mwezi wa Disemba ilikuwa haikwepeki si kwa hapa Zanzibar tu bali hata katika nchi mbali mbali za Afrika na Ulaya.

About Zanzibar Daima 1606 Articles
Zanzibar Daima, Jana, Leo na Kesho

Be the first to comment

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.