News Ticker

Bodi ya mikopo ya elimu ya juu Tanzania yatangaza vita kwa wadaiwa sugu


Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imewataka wanufaika wote wa mikopo ambao wanadaiwa na hawajaajiriwa bado, kufika katika ofisi za bodi hiyo zilizoko katika maeneo mbalimbali nchini, ili kupewa maelekezo na utaratibu wa namna ya kulipa mikopo yao.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Bodi ya Mikopo zilizoko Mwenge, Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa  bodi hiyo, Abdul-Razaq Badru amesema:

“Tunatoa wito kwa wale ambao kwa sababu fulani fulani walikuwa hawajaanza kulipa, walipe na wanakaribishwa kwenye ofisi zetu. Hata wale ambao hawako kwenye ajira maalum kuna utaratibu maalum tumewatengenezea. Wanaweza kuwasiliana na sisi katika mawasiliano yetu au wakaja ktika ofisi za Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza, Arusha, Zanzibar na kwingineko il tuwape maelekezo na utaratibu maalum wa kulipa.” amesema Mkurugenzi Badru

Jengo la Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu nchini (HESLB) lililopo jijini Dar es Salaam

Aidha Mkurugenzi Badru amesema bodi haitosita kuwashughulikia  wale wote ambao hawajarejesha mikopo yao ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua kali za kisheria sambamba na kuwafikisha mahakamani.

“Mtu yeyote aliyekopa mkopo kwa ajili ya kusoma, njia pekee ya kisheria inayoweza kumfanya asilipe mkopo huu, ni labda awe amefariki. Lakini kama umekopa, uko hai, uko hapa nchini na hata ukienda nje, sisi ni lazima utalipa huo mkopo kwa gharama yoyote ile,” amesisitiza.

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi Urejeshaji wa Mikopo, Phidelis Joseph amewataka wale ambao tayari wameshaanza kurejesha madeni katika akaunti za benki za Bodi ya Mikopo, waweke maelezo yote katika ”pay-in-slip’ zao.

“Wale wanufaika ambao wanajitokeza na wanalipa kwenye zile ‘bank accounts’ zetu waweke ‘details’ zote. ‘Unapodeposit’ unatakiwa utoe taarifa kwa Bodi ya Mikopo kwamba nimeweka pesa. Lakini vie vile unapoiandika ile ‘slip’ yako uiandike vizuri..,” amesema Phidelis Joseph.

Vile vile amewataka wanufaika wa mikopo ambao wameshaanza kulipa, wafike katika ofisi za Bodi ya mikopo ama kutumia mitandao ya Bodi, kwaajili ya uhakiki.

About Zanzibar Daima (1550 Articles)
Zanzibar Daima, Jana, Leo na Kesho

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s