News Ticker

Mama wajawazito watakiwa kujifungulia hospitali


Waziri wa nchi afisi ya Rais Tawala za mikoa na idara malumu za SMZ  Haji Omar Kheri amewataka kinamama kujifungulia Hospitali na kuacha mazoea ya kujifungulia nyumbani ili kuepuka matatizo yanayoweza kujitokeza.
Waziri Kheria ameyasema leo katika kituo cha Afya cha Sebleni wakati wa uzinduzi wa Wodi ya wazazi ya kinamama wa zaidi ya shehia saba ikiwa ni mwendelezo wa shamara shamara za miaka 54 ya mapinduzi ya Zanzibar.
Amesema kinamama kujifungulia hospitali kuna wapa asilimia kubwa kuzaa salama kwani inapotokea tatizo inakuwa ni rahisi kulitatua,kuliko kujifungulia nyumbani.
“Nakuombeni acheni kujifungulia nyumbani kwa sababu nyumbani hakuna utaalamu wa kutosha na likitokea tatizo ni vigumu kulikabili”alisema Waziri huyo.

Haji Omar Kheri: Waziri wa nchi afisi ya Rais Tawala za mikoa na idara malumu za SMZ 

Akijibu changamoto ya kutoajiriwa wafanyakazi wanao jitolea kituoni hapo  kwa kipindikirefu ameitaka Ofisi ya mkoa,wilaya na manispaa kulitatua tatizo hilo kwa kulifikisha idara ya uajiri ili ufumbuzi wa ajira upatikane.
Naye mkuu wa mkoa wa mjini magharibi Ayub Muhamed Mahmud amesema kuwa kufunguliwa kwa wodi hiyo nifrusa ya kipekee kwa mkoa huo una idadi kubwa ya wazazi wanao kwenda hospital ya mnazi mmoja hospitali kujifungua.
Amesema malengo na dhamira ya mapinduzi ya Zanzibar ni kuwaondolea wananchi matatizo yanayo husiana na huduma za kijamii ikiwemo Afya,maji,elimu hivyo ni jukumu la wananchi kuzidisha mashirkiano kwa serikali yao.
Naye Mkurugenzi Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Jamala Adam Taib alisema ujenzi wa wodi hiyo ni msaada wa Shirika la DANIDA na UNFPA kujenga ukuta na kutoa vifaa tiba.
Wodi hiyo ya Wazazi kwa sasa itakuwa inazihudumia shehia saba ikiwemo Sebleni, Amani,Kilimahewa, Magogoni, na Kwamtipura.
About Zanzibar Daima (1550 Articles)
Zanzibar Daima, Jana, Leo na Kesho

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s