Mohammed Aboud: Lengo la mapinduzi ni kuwafikishia huduma bora wananchi

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Mohamed Aboud Mohamed, amesema ujenzi wa barabara ni kiungo muhimu katika kuharakisha maendeleo kwa wananchi hasa wanaoishi maeneo ya vijijini.

Alisema barabara huongeza ajira, na kuinua kipato cha wananchi sambamba na kusaidia kusafirisha mazao yao na kupeleka sokoni kwa urahisi mkubwa.

Aboud ameyasema hayo huko kisiwani Pemba wakati akizindua barabara ya Madenjani-Mzambaruni yenye urefu wa KM 5, ambayo imegharimu shingi Bilioni 1.96, na kubainisha kuwa ujenzi huo ni miongoni mwa Matunda ya Mapinduzi ya mwaka 1964.

Aidha alisema moja ya malengo makubwa ya waasisi wa Mapinduzi ni kuwafikishia wananchi huduma bora na muhimu, ikiwemo Maji safi na Salama, elimu bure, matibabu bure na huduma za usafiri ikiwemo barabara za kisasa.

Sambamba na hilo  alisema Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji, kwa sasa ina mpango wa kununua meli mbili kubwa, ikiwemo ya mafuta pamoja na meli ya abiria na Mizigo, itakayoweza kuwahudumia wananchi wa Unguja na Pemba.

Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Balozi Ali Abeid Karume, alisema Wizara yake itaendelea kuzifanyia ukarabati na kuzijenga upya barabara mbali mbali za Unguja na Pemba, ili kuhakikisha wananchi wanaondokana na usumbufu wa huduma za usafiri.

Alisema Wizara ipo katika hatua za kuyafanyia ukarabati mkubwa, majengo yote ya yaliyojengwa na Muwasisi wa Mapinduzi Mzee Abeid Amani Karume, ili kuyarudisha katika hadhi yake kama yalivyoachwa na muwasisi huyo.

About Zanzibar Daima 1613 Articles
Zanzibar Daima, Jana, Leo na Kesho

Be the first to comment

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.