Kikao cha marais wa Afrika Mashariki kuamua khatma ya biashara ya mitumba Zanzibar

Hatma ya matumizi na uingizwaji wa nguo za mitumba visiwani Zanzibar inatarajiwa kupatikana baada ya kikao kitakachofanyika mwezi Februari huko nchini Uganda, kikao ambacho kitawakutanisha marais wa Jumuiya ya nchi za Afrika Mashariki.

Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Zanzibar, Balozi Amina Salum Ali aliyasema hayo wakati akitoa ufafanuazi juu ya marufuku iliyotolewa na Serikali ya Zanzibar juu ya uingizwaji wa bidhaa hizo huko Ofisini kwake Migombani nje kidogo ya mji wa Zanzibar.

Amesema awali Serikali ya Zanzibar kupitia Wizara hiyo ilipiga marufuku ya uingizwaji wa bidhaa ya nguo za mitumba kuwa mwisho kuingia visiwani humu ni mwaka 2018, lakini kutokana na migongano baina ya nchi za Afrika, Zanzibar imeshindwa kutekeleza agizo hilo kama ilivyokusudiwa.

Aidha alisema kuwa kabla ya kufikiwa kwa maamuzi hayo nchi za Afrika Mashariki zimepiga marufuku ya uingizwaji wa nguo hizo ila uongozi wa Marekani ulionekana kupingana na maamuzi hayo kwa nchi za Afrika kwa kuonesha nia ya kutoridhishwa na hatua hiyo.

“Lakini kuna nchi za Afrika kama Kenya wao wanaendelea na marufuku ya mitumba nchini mwao ila sisi tumeona bora tuungane na wengine kwa kuangalia njia mbadala’ alisema.

“Baada ujumbe wetu huo kurejea Afrika ulikutana na mawaziri  na kutoa mapendekezo waliyoyapata nchini huko ila Mawaziri walilazimika kufikia maamuzi ya kuwa marais ndio watakaokuwa waamuzi wa mwisho juu ya suala hilo” alisema.

Hivyo alisema kuwa kinachosubiriwa hivi sasa ni kikao cha marais hao ambacho ndicho kitakachotoa muongozo sasa wa uingizwaji wa bidhaa hizo, bila ya kutaja mazungumzo yaliofikiwa kati ya ujumbe wa Afrika uliotumwa Marekani na viongozi husika wa nchi hiyo.

About Zanzibar Daima 1611 Articles
Zanzibar Daima, Jana, Leo na Kesho

Be the first to comment

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.