Abu Dhabi yaahidi neema kwa Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amefanya mazungumzo na Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan, mrithi wa mtawala wa Abu Dhabi na Naibu Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi wa Nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

Katikamazungumzohayoviongozihaowalikubalianakwapamojakuendelezauhusiano na ushirikiano wa kidugu na kihistoriauliopokwamuda wa miaka 44 hivisasahatuaambayoUmeletamanufaamakubwakwapandezotembilikatikasekta za maendeleozikiwemo za kijamii na kiuchumi.

Viongozi hao walifanya mazungumzo hayo katika ukumbi wa Makaazi ya Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan, mjini Abu Dhabi, mazungumzo yaliyohudhuriwa na viongozi mbali mbali wa ngazi za juu wa Abu Dhabi wakiwemo Mawaziri, Spika wa Abudhabi pamoja na viongozi wengine wa ukoo wa Sheikh Zayed (UAE) pamoja na wageni waalikwa.

Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan, kwa upande wake alimuhakikishia Dk. Shein kuwa Abu Dhabi ataendelea kuiunga mkono Zanzibar na yuko tayari kutoa ushirikiano wake katika kuimarisha sekta za maendeleo zikiwemo za kiuchumi na kijamii.

Aidha, Sheikh Mohammed, alieleza kuwa Abu Dhabi inathamini sana uhusiano na ushirikiano huo na iko tayari kuunga mkono vipaumbele vyote vilivyowekwa na Zanzibar katika kuimarisha miradi mbali mbali ya maendeleo.

Kwa upande wake Dk. Shein, alitumia fursa hiyo kumpongeza na kumshukuru  Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan, kwa mualiko wake aliompa nchini humo pamoja na mapokezi makubwa aliyoyapata yeye na ujumbe wake na kueleza kuwa ziara hiyo ni kichocheo kikubwa cha mashirikiano kati ya Zanzibar na Abu Dhabi.

Dk. Shein alieleza kuwa Zanzibar ina mengi ya kujifunza kutoka kwa ndugu zao wa Abu Dhabi hasa ikizingatiwa kuwa nchi hiyo imepiga hatua kubwa katika sekta zote za kiuchumi, kijamii na nyenginezo.

Wakati huo huo, Rais Dk. Shein alifanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo ya Abu Dhabi katika ukumbi wa Hoteli ya Kimataifa ya “Jumeirah Etihad Towers” mjini Abu Dhabi ambapo katika mazungumzo hayo Mkurugenzi huyo alimueleza Dk. Shein azma ya Mfuko huo katika kuiunga mkono Zanzibar.

Katika maelezo yake, Mkurugenzi huyo alieleza kuwa Mfuko huo uko tayari kuunga mkono juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuimarisha miradi ya maendeleo ikiwemo miundombinu pamoja na miradi mengine ya kijamii na kiuchumi.

Naye Dk. Shein kwa upande wake aliupongeza Mfuko huo kwa kuonesha kuwa tayari kuiunga mkono Zanzibar katika kuendeleza miradi yake ya maendeleo huku akieleza historia ya Mfuko huo katika kuiunga mkono Zanzibar.

Mapema Dk. Shein akiwa na ujumbe wake akiwemo Mama Mwanamwema Shein, alitembelea Mji mpya wa kisasa wa Masdar unaoendelea kujengwa kwa dhamira ya kuufanya kuwa ni mji wa kipekee duniani unaotumia nishati mbadala hasa umeme wa jua katika shuhuli zake zote zinazohitaji nishati.

Akiwa katika mji huo ulioko umbali wa kilomita 17 kutoka mjini Abu Dhabi, Dk. Shein alipata maelezo kutoka kwa uongozi wa Mradi huo Mkurugenzi Mkuu Yousef Baselaib na Meneja Msaidizi wa Mradi huo Fatma Al Shaigy walimueleza dhamira ya ujenzi huo ikiwa ni pamoja na kuendeleza miji inayoweka uhifadhi wa mazingira kwa kutumia nishati mbadala duniani na kumtajia nchi ambazo tayari zimeanza kufaidika na teknolojia hiyo kupitia taasisi yao.

Pia, alitembelea Msikiti Mkuu wa Abudhabi ambao unajulikana kwa jina maarufu la “Sheikh Zayed Grand Mosque” na kusali sala ya Adhuhuri, ambapo Dk. Shein akiwa katika msikiti huo alidhuru kaburi la Baba wa Taifa hilo na muwasisi wa Muungano wa nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Marehemu Sheikh Zayed bin Sultan Al Nahyan, na kumuombea dua.

About Zanzibar Daima 1613 Articles
Zanzibar Daima, Jana, Leo na Kesho

Be the first to comment

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.