Maseneta Marekani wakubaliana kufungua tena shughuli za Serikali Kuu

Baraza la Senate la Marekani limefikia makubaliano ya kupitisha kwa mpango wa matumizi na kuifungua tena serikali kuu baada ya kufungwa kwa baadhi ya shughuli za serikali kwa siku tatu.

Wademocrat 33 walijiunga na Warepublican 48 kumaliza mjadala katika baraza la senate lenye wanachama 100 kuongeza muda kwa mswaada wa matumizi ya serikali kuu mpaka Februari 8. Hatua hiyo ya haraka ilitarajiwa kwenda kwenye Baraza la Wawakilishi, na baada ya hapo mswaada utakwenda White House kwa Rais Donald Trump ili kuutia saini.

Zaidi soma hapa.

About Zanzibar Daima 1613 Articles
Zanzibar Daima, Jana, Leo na Kesho

Be the first to comment

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.