HABARI

Ujenzi wa maduka ya kisasa Michenzani Zanzibar kuanza ndani ya 2018

Ujenzi wa maduka makubwa ya kibiashara ya kisasa (SHOPPING MALL) Michenzani muembe Kisonge unatarajia kuanza rasmi baada ya kupatikana mshauri muelekezi na mkandarasi wa eneo hilo.

Hayo yamebainishwa na Ofisa Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) Mussa Yussuf wakati alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusiana na ujenzi huo huko ofsini kwake Kilimani Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.

Alisema hivi sasa wamo katika hatua ya mwisho ya kufungua tenda ya kumpata mshauri elekezi na Mkandarasi na kusema mara baada ya kukamilika kwa hatua hiyo, ujenzi huo utaanza rasmi ndani ya mwaka huu wa 2018.

Aidha alisema kuwa ujenzi huo ulikuwa uanze  mwaka jana lakini imeshindikana kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo kufuatwa kwa  taratibu za manunuzi na muda, kupima aina ya udongo uliopo katika eneo husika, na kima cha maji kutokana na ardhi iliyopo hatua ambazo zitamuelekeza mkandarasi kujua jengo hilo litakavyokuwa.

Pia aliongeza kuwa, kila kampuni inayojenga inatakiwa ifanye upembuzi yakinifu ambao hautoharibu mazingira ya watu wengine waliokaribu na eneo smabmba na ubora wake.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.