Kenya yaingia katika historia ya dunia kwa kuunda satalaiti yake

Kenya imetangaza kuunda satalaiti yake ya kwanza ikiwa ni mafanikio makubwa kwa nchi hiyo ya Afrika Mashariki katika uga wa sayansi ya anga za mbali.

Satalaiti hiyo ndogo iliyogharimu zaidi ya dola milioni moja ina muundo wa nanosatellite na itarushwa katika anga za mbali mwezi Aprili au Mei kutoka katika Kituo cha Kimataifa cha Anga za Mbali.

Taarifa zinasema satalaiti hiyo ambayo itakuwa na jukumu la kuchunguza shughuli za kilimo na kuangalia eneo la pwani, imeundwa na Chuo Kikuu cha Nairobi na Shirika la Anga za Mbali la Japan.

Chuo Kikuu cha Nairobi kinasema satalaiti hiyo ndogo ya sentimeta 10 kwa 10 itatumika kufanyia majaribio tekenolojia za kuunda satalaiti kubwa zaidi katika siku za usoni.

Iwapo satalaiti hiyo itarushwa angani kwa mafanikio basi Kenya itakuwa imejiunga na kundi la nchi chache za Afrika amabzo zimerusha satalaiti katika anga za mbali ambazo ni Afrika Kusini, Nigeria, Ghana, Algeria na Misri.

Sataliti hiyo imepewa jina la 1KUNS-PF (Kenyan University Nano Satellite Precursor Flight) na udogo wake umeifanya kuwa ya kipekee.

Chanzo: Parstoday Kiswahili

About Zanzibar Daima 1613 Articles
Zanzibar Daima, Jana, Leo na Kesho

Be the first to comment

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.