Jaji Makungu: Tumefanikiwa lakini tunakabiliwa na changamoto

Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu  amesema uwendeshaji wa kesi kwa mwaka uliomaliza hakuwa mbaya na kwa kiasi Idara ya Mahakama imefanikiwa katika utekeleza wa majuku yake.

Hayo ameyasema leo huko Ofisini kwake Vuga  mjini Zanzibar wakati akizungumza na Wandishi wa habari kuelekea maadhimisho ya wa wiki ya sheria duniani ambayo kilele chake hufanyika February 12 ya kila mwaka.

Amesema pamoja na changa moto zinazoikabili Idara ya Mahakama lakini wamefanikiwa kuzitolea hukumu kesi mbalimbali ikiwemo za udhalilishaji na madawa ya kulevya.

Aidha ameongeza kuwa, licha ya wananchi wengi kulalamikia Idara hiyo kwa kushindwa kutoa hukumu kwa wakati lakini changamoto kubwa inayojitokeza ni kushindwa kutoa mashirikiano ipasavyo hasa katika kutoa ushahidi.

Hivyo Jaji Makungu  amewataka wananchi kutoa ushirikiano  ipasavyo ikiwemo kutoa ushahidi kila inapohitajika ili kuwatia hatiani wale wanaofanya makosa na jinai mbalimbali.

Akizungumzaia kuhusu shamra shamra za maadhimisho hayo Jaji Makungu amesema wanatarajia kufanya maonesho ya siku tatu kuazia February 9 hadi 11 katika viwanja vya maisara.

Pia amesema  kilele cha sherehe hizo zitafanyika baraza la wakilishi la zamani na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa rais wa Zanzibar Dkt. Ali Muhamed Shein ambapo Ujumbe wa mwaka huu ni “Kuimarisha Utwala Wa Sheria na Uchumi”.

About Zanzibar Daima 1613 Articles
Zanzibar Daima, Jana, Leo na Kesho

Be the first to comment

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.