SIASA

Wazanzibari ‘wanaoushitaki’ Muungano wahofia maisha yao

Kiongozi wa kundi la Wazanzibari 40,000 waliofunguwa kesi kwenye Mahakama ya Afrika Mashariki kuhoji uhalali wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Rashid Salum Adi, anasema anakhofia usalama wa maisha yake na sasa ameuomba Umoja wa Mataifa kumpa ulinzi yeye na viongozi wenzake ili waweze kushiriki kikamilifu kwenye kesi hiyo.

Katika barua aliyouandikia Umoja wa Mataifa na nakala yake kuonekana na Zaima Media, Adi anasema serikali na vyombo vyake, ambao ni walalamikiwa kwenye kesi hiyo inayoanza rasmi tarehe 8 Machi 2018 mjini Arusha, wameanza kutumia mbinu za kutaka kuwazuwia kufika mahakamani.

Barua ya Wazanzibari 40,000 kwa Umoja wa Mataifa

 

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.