UTAMADUNI

Mbunge Ally Saleh achapisha diwani nyengine ya ushairi

Mwandishi wa habari aliyesomea sheria na kugeuka kuwa mwanafasihi na kisha mwanasiasa, Ally Saleh (Alberto), amechapisha diwani yake nyengine ya ushairi, inayoitwa ‘TUPO: Diwani ya Tungo Twiti’, ambayo ni mkusanyiko wa tungo zilizowahi kutumwa kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter.

Licha ya kuandikwa kwake kwa lugha ya kifasihi, tungo hizi zina ujumbe mkali wa kisiasa, kwani zimeandikwa¬†katika “kipindi kigumu katika siasa za Tanzania ambapo demokrasia imeonekana kuzongwa na moshi angani na mbigili ardhini”, anasema mbunge huyo wa Malindi kisiwani Unguja, akiongeza kwamba: “Ni kipindi cha matukio mengi na mengi yao yamenaswa katika diwani hii. Ni kipindi ambacho nikiwa katikati ya muda wangu wa kutumikia Bunge, nikiwa Mwakilishi wa wananchi wa Jimbo la Malindi, Zanzibar nikiona nimeingia siasani kipindi kizito sana.”

Diwani hiyo inapatikana kwenye maduka yote ya mtandao wa Amazon kuanzia leo. Kuagizia, tafadhali bonyeza hapa.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.