Hatimaye Nondo apandishwa kizimbani kiutata

Hatimaye jeshi la polisi nchini Tanzania limempandisha kizimbani kiongozi wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Mahmoud Abdul Nondo, mkoani Iringa, baada ya takribani wiki mbili za kumshikilia. Taarifa zinasema kuwa alisafirishwa usiku wa jana (Machi 20) kutoka Dar es Salaam kwenda Iringa, ambako leo amesomewa mashitaka mawili mahakamani – la kusambaza taarifa za uongo zenye maneno “Am at high risk” kwa lengo la kupotosha kinyume na kifungu cha 16 cha sheria ya makosa ya mitandao na la kutoa taarifa za uongo kwa mtumishi wa umma kwamba alitekwa kinyume na kifungu cha 122(1) cha Kanuni ya Adhabu.

About Zanzibar Daima 1613 Articles
Zanzibar Daima, Jana, Leo na Kesho

Be the first to comment

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.