Mahakama yampa dhamana Nondo, lakini askari magereza wakimbia naye

Habari za hivi punde kutoka Mjini Iringa zinasema kuwa Mahakama mkoani humo imekubali kutoa dhamana kwa kiongozi wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Mahmoud Nondo, ikiagiza masharti ya dhamana hiyo kutimizwa ndani ya kipindi cha masaa matatu, lakini inaropitiwa kuwa askari wa jeshi la Magereza wameondoka naye na kwenda naye gerezani ndani ya kipindi cha nusu saa tu tangu uamuzi kutolewa.

Mawakili wa Muungano wa Watetezi wa Haki (THRDC), Kituo cha Haki za Binaadamu na Sheria (LHRC) na TSNP wanaendelea muda huu kupigania utekelezaji wa masharti ya dhamana kama ilivyo amri halali ya mahakama.

About Zanzibar Daima 1613 Articles
Zanzibar Daima, Jana, Leo na Kesho

Be the first to comment

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.