HABARI

Maalim Seif hajashindwa kuirejesha haki ya Oktoba 25 – Jussa

Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa CUF, Ismail Jussa, amesema kuwa katibu mkuu wa chama chake, Maalim Seif Sharif Hamad, bado hajashindwa hadi sasa kuirejesha haki yao iliyoporwa ya ushindi wa uchaguzi wa tarehe 25 Oktoba 2015 na kwamba anaendelea na juhudi za kidiplomasia kuirejesha, hadi hapo atakapoona kwamba hakuna uwezekano wa kupatikana tena na ndipo atakapowaachia Wazanzibari wenyewe cha kufanya. Jussa aliyasema hayo kwenye kipindi cha ULINGONI kinachorushwa na kituo cha televisheni cha Island TV kilichopo Mjini Unguja, ambacho kilikuwa kinathmini hali ya kisiasa visiwani Zanzibar.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.