Miguna Miguna azuia kupandishwa ndege kwa nguvu

Mwanasheria na mwanaharakati wa Kenya mwenye uraia pia wa Canada, Miguna Miguna, amezuia operesheni ya kumpandisha ndege kwa nguvu kumpeleka Dubai iliyochukuliwa na mamlaka za uhamiaji na vyombo vya usalama vya Kenya usiku wa jana (26 Machi 2018), katika mkasa wa aina yake uliosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na vyombo kadhaa vya habari. Awali Miguna alikataliwa kuingia nchini Kenya, huku idara ya Uhamiaji ikimkata kwanza aombe kibali cha kuingia nchini humo, taifa ambalo alizaliwa, kukulia na ambalo mwenyewe anasema hajakana uraia wake.

 

About Zanzibar Daima 1613 Articles
Zanzibar Daima, Jana, Leo na Kesho

Be the first to comment

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.