Kulala viongozi sita rumande haijapata kutokea-Zitto

Baada ya viongozi sita wa ngazi ya juu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) akiwemo Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe kukosa dhamana jana na  kurudishwa rumande.

Mbunge wa Kigoma mjini na kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe amefunguka kwamba tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi hajapata kuona tukio la kusekwa ndani thuluthi mbili ya viongozi wa kitaifa wa chama kikubwa cha pili cha siasa nchini kwa pamoja.

Ameyasema hayo kupitia ukura wake wa kijamii mara baada ya kutoka mahakama ya hakimu mkaazi Kisutu, alipohudhuria ili kusikiliza kesi zinazowakabili viongozi hao wa Chadema.

Amewaonya Watanzania kwamba mfumo wa vyama vingi upo hatarini kubomolewa, akishangaa ukimya usio na kifani wa wanachama wa vyama ya upinzani nchini.

Viongozi hao ni Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe, Katibu Mkuu wa Chama, Dkt Vincent Mashinji, Mbunge wa Iringa mjini, Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu, John Mnyika,  Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu na Mweka Hazina wa Baraza la Wanawake la Chama hicho, Esther Matiko.

Viongozi hao wamesomewa mashtaka nane ikiwemo ya kufanya maandamano yaliyosababisha kifo cha Mwanafunzi wa chuo cha NIT, Akwilina Akwiline .

Viongozi hao  walinyimwa dhamana jana na kurudishwa rumande hadi kesho watakapo rudishwa tena mahakamani ili kutolewa maamuzi ombi lao la kupatiwa dhamana.

About Zanzibar Daima 1613 Articles
Zanzibar Daima, Jana, Leo na Kesho

Be the first to comment

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.