HABARI

Mambosasa asema aliyemuua Akwilina bado hajajuulikana

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa ameviambia vyombo vya habari aliyemuua Mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini bado hajajuulika na uchunguzi unaendelea.

Mambosasa ameyasema hayo  leo wakati akijibu swali la mwandishi wa habari juu ya maendeleo ya uchunguzi wa mauaji ya Akwilina yaliyotokea wakati Polisi ikitawanya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), katika eneno la Kinondoni jijini Dar es Salaam.

“Mpaka sasa bado haijabainika ni silaha gani ilitumika hadi kumpata Akwilina kwa sababu Askari walikuwa wengi siku ile na hakukuwa na ushahidi ni yupi aliyetenda kosa hilo”, amesema Mambosasa

Amesema upelelelezi bado haujakamilika na ukiwa tayari umma utataarifiwa.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.