Sasa nchi ina udikteta kamili-Mbowe

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, (Chadema) Feeman Mbowe ametoa kauli  kwamba Tanzania sasa ina udikteta kamili.

Kuali ya Mbowe imekuja masaa machache baada ya kutoka rumande kwa kukamilisha taratibu za kupewa dhamana, akiwa na wenzake sita ambao wengi ni viongoz wa ngazi ya juu wa Chadema.

“Ambacho naweza kuzungumza kwa sasa, ni kuwa zamani tuliona nchi hii ikiwa na udikteta uchwara lakini kwa sasa nchi hii ina udikteta kamili”, amesema wakati akizungumza na vyombo vya habari.

Kwa upande mwengine Mbowe amesema wameonana na Watanzania zaid ya elfu mbili katika gereza la Segerea ambao wengi wao, haki zao zimecheleweshwa na kuminywa.

 

About Zanzibar Daima 1613 Articles
Zanzibar Daima, Jana, Leo na Kesho

Be the first to comment

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.