AFRIKA, HABARI

Congo yathibitisha mripuko mpya wa Ebola

Serekali ya Congo imetangaza mripuko mpya wa ugonjwa wa Ebola baada ya kuthibitishwa watu wawili kukutwa na virusi ya ugonjwa huo na takribani 17 kufariki Kaskazini-Magharibi mwa taifa hilo.
“Nchi yetu imekumbwa na mripuko wa virusi vya Ebola ambapo vinatishia usalama wa afya za watu wetu”, amesema .

Waziri wamesema sample za watu watatu zilipelekwa katika taasisi ya kitaifa ya uchunguzi wa kibayalojia Kinshasa, wawili wamegundulika kuwa na virusi wakitokea jimbo la Equateur.

Kabla ya mripuko huo kuthibitishwa, maafisa wa afya katika maeneo hayo waliripoti juu ya wagonjwa 21 wenye dalili ya homa ya Ebola na kumi na saba kati yao waliaga dunia.

Miaka kadhaa nyuma wakati wa mripuko mkubwa wa ugonjwa huo kaskazini mwa Afrika, nchi ya Kongo ilipoteza watu wanne kati ya nane walioathirika.

Waziri wa afya amesema, ataalamu wa afya wanatarajiwa kufika maeneo yaliyoathirika leo kuweka mikakati ili kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.