Bendera ya Marekani yachomwa Bungeni

Hasira zinaendelea kushamiri baada ya uwamuzi wa rais wa Marekani Donald Trump kujiondoa katika makubaliano ya nyuklia yaliyowafikiwa kati ya Iran na mataifa sita yenye nguvu duniani.

Asubuhi ya leo wabunge katika bunge la Iran wameichoma moto bendera ya Marekani wakiwa mubashara katika runinga wakati bunge la nchi hiyo likiendelea na vikao vyake.

Katika video iliyosambaa inawaonesha wabunge kadhaa wakiichoma moto bendera hiyo iliyo katika karatasi huku wakipiga kelele “Kufa kwa Marekani”, pia taarifa zinaeleza wameichoma moto karatasi iliyokuwa na mkataba wa makubaliano ya nyuklia.

Wakati kuchomwa kwa bendera ya Marekani ni kitu cha kawaida katika taifa la Iran lakini wachunguzi wa mambo wamedai kwamba hii ni mara ya kwanza bendera ya Marekani kuchomwa ndani ya Bunge na Iran.

About Zanzibar Daima 1613 Articles
Zanzibar Daima, Jana, Leo na Kesho

Be the first to comment

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.