MCHAMBUZI MAALUM, SIASA

Happy Birthday CCM!


Imenichukuwa dakika tano tu hivi hadi kuwaza niandike nini kama sehemu ya zawadi kwa chama changu na marafiki zangu wa chama cha Mapinduzi CCM! Nimeona ni kheri kuandika kwa sababu si wote wenye uwezo wa kuja mbele ya hadhara hii na kuimba ule wimbo maarufu wa “Happy Birthday!”

Najuwa tumewakosesha uhondo, lakini ni nani angeweza kuwa tayari kubeba gharama ya nauli ya wao kuwarejesha makwao? Jibu ni hapana,  kwa sababu licha ya hamu na ghamu yakutaka kuwa nao katika kuikata keki hii pamoja ila hali za mifuko yetu haziruhusu hata kama mtoto huyu asherehekewae leo ni wakitajiri!

Ndio miaka 42 sio kidogo. Ni wajibu kuitangaza na ikibidi kuisherehekea. Tofauti pekee ni namba ya umri na muonekano wa part yenyewe. Tungeweza kuisherehekea hata kwa sote kujifungia ‘Prison Island’ au nyumbani mwetu pale Mapinduzi Squre! Sehemu moja tulivu na iliyobeba kumbukumbu nzuri ya makuzi ya mtoto mwenyewe (CCM). Ndio maana nikaona kheri kuandika kuliko kusema nipike keki ambayo huenda matokeo ya ukataji wake ikawaweka wengine mbali maana ndani yetu wapo wenye kisukari!

Cha kufurahisha ni kuona sherehe imepata watoto! Ila ni kawaida kwa sababu tupo kwenye ‘happy birthday‘. Sisitizo kuu ni njia ya kuwatawanya. Naam, inahitaji hekima na busara katika kuwambia hao watoto kuwa hatutokuwa na zoezi la kukata keki kwa mawaka huu. Sababu tutawapa baadae!

Tangu kumalizika kwa mwaka wa 2015 ‘style’ ya maisha yetu yalibadilika. Inawezekana yamekuwa bora zaidi. Tukaizungushia kuta nyumba yetu kwamba hadi paa la nyumba ikawa tabu kwa jirani kuliona. Hatukujali kitu ujirani mwema. Ya kwetu ya kawa yetu na yao yakawa yao. Tukiwa ndani ya jumba la kifahari ila lisilojiruhusu kuonekana na wapita njia tukawa sisi tunangalia ‘Move’ ile inayoitwa ‘dectator’ huku mdada wa kazi jikoni akiperuzi kile kitabu alichomalizia nacho masomo kijijini kwao kinachoitwa ‘This Time Tomorrow’. Baba wala sisi watoto hatukuwahi kujuwa kuwepo kwa kitabu hichi nyumbani! Tulichokuwa tukijuwa sisi ni kumiliki jumbwa kubwa na lililozungushiwa uzio usioweza kupenyeza sauti za majirani wetu wa kufikia mule ndani! Tukajidanganya. 

Uwepo wa ‘This Time Tomorrow’ ndani ya viganja vya mdada wa kazi ndani kukampatia marafiki wa kusemeshana nae. Kuanzia Asinjo, Wanjiro, Strenger, Shoemaker hadi police officer! Ikawa tumepata tena sauti tusioiwazia! Matokeo yake ndani hamukaliki kutokana na vuguvugu la kudai uhuru wa ushirikishwaji wa wananchi na ambao awali tulishapingana nao. Somo zito!

Ni kama niingaliavyo CCM leo hii na miaka yake 42 ya kuzaliwa kwake. Kwa CCM Zanzibar hii ilipaswa kuwa siku muhimu sana dhidi ya Wapinzani wake kisiasa. Ndani ya kuitazama miaka 42 ya kuzaliwa kwake kimyakimaya hakuwezi kuwafurahisha wanaojiita Wahafidhina. Tulipaswa kukesha nao kitaifa, ili asubuhi ya kesho tuamkie na maadhimisho yetu kwa ‘style’ ile ile ya maandamano, chuki na vijembe visivyo na mfano.

Hali hii ya ukimya sisi hatukuizoea ukizingatia siasa ya Visiwani ni mguu supu licha kwamba timu pinzani siku zote hulimiliki dimba iwapo zitafuatwa zile sheria kumi na nane za mchezo wenyewe.  Sasa sijui ni nani hapa wa kulaumiwa maana tuliopiga marufuku miikutano ya kisiasa ni sisi wenyewe! Na huu ulikuwa mtego!

Sawa wapo watakao sema halii hii imeshazoeleka kwa Wana-CCM tangu kuingia madarakani kwa Raisi John Pembe Magufuli, kutokana na maamuzi yake ya kuzighairisha baadhi ya sherehe za Chama na baadhi ya zile za kiserikali.

Ila ni vizuri watu wakafahamu kuwa kutimia kwa miaka 42 ya CCM inawatambulisha zaidi Wahafidhina kuliko waasisi wa Tanu na ASP ambayo leo ndio CCM yenyewe. Wahafidhina ni kikundi cha Watu ndani ya CCM kilichofanikiwa kuhodhi akili na mitazamo ya Vijana wengi ndani ya Chama. Ni rahisi ukiwaita ‘Wapiga dili’ ambao huishi kwa matukio. Kwa sababu ya nguvu yao wakisaidiwa na baadhi ya walio ndani ya madaraka kwa upande wa pili wa mungano hili la kutokuwa na maadhimisho ya kitaifa hawalipendi. Kusudio lao ni kupata jukwaa la kuonekana kwa kutumia kivuli fikirishi cha kiitwacho ‘Maendeleo’!

Inawezekana wanayo hoja. Ila kilichopo katika Vichwa vya wale wenye mrengo wa wastani ni utetemeshi wa kuipokea tafsiri ya Mahakama na jumuiya za kimataifa kati ya ipi ni shughuli za kisiasa na upi haihusiani na shughuli za kisiasa wakati shughuli zote kwa vyama vyote eti tumevizuia visifanye mikutano ya kisiasa!

Happy birthday chama changu!

This time Tomorrow!

Tanbihi: Makala hii imeandikwa na Abdulwahab Mohammed.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.