LUGHA

Kama kichwa cha treni

Naendeshwa, kama kichwa cha treni Hidogoshwa, kama yaya wa nyumbani Hichezweshwa, kama vile punguani Hiamka, ni mbio kutwa ni njiani Hekaheka, za kutisha insani Hivunjika, wananitupa jaani Niendako, huwa mimi sikuoni Mara huko kushoto na Endelea

LUGHA

Ishangia Ramadhani

Ishangia Ramadhani, nianze fanya hashuo Nijiweke kiblani, hijifanya mwanachuo Ilhali ni shetani, nawavua watu nguo Ikingia Ramadhani, mimi hujifanya mwema Nikalisha majirani, wanyonge na mayatima Japokuwa maluuni, hukaa hashika tama Hujifanya Muungwana, wachafu nikawabeza Haacha Endelea

LUGHA

Mimi ni Profesa

Mimi ni Profesa, nina PhD ya Political Science Na ng’ombe wa maziwa, na magari ya kubeba kifusi Nyumbani kwangu hakuna vitabu, kuna nyasi Mara ya mwisho nilisoma Chuo cha Barkley Waendako watu teule Nimerudi kwetu, Endelea