MCHAMBUZI MAALUM, SIASA

Maalim Seif na Jahazi la Nuh

Kinachoendelea hivi sasa katika siasa za Tanzania, kwa ujumla, hasa kwa upande wa Zanzibar katika Chama Cha Wananchi (CUF) kimenifanya nikumbuke tarekhe za visa vya Mitume na kwa muktadha wa makala hii fupi nitaangalia kazi kubwa ya kiutume iliyofanywa na Nabii Nuh (AS), upinzani aliokumbana nao na mwisho kulitazama Jahazi la Uokozi aililolichonga kwa amri… Continue reading Maalim Seif na Jahazi la Nuh

MCHAMBUZI MAALUM, SIASA

JPM ameshinda walau kwa sasa

“LINI?”  Ni swali nililojiuliza, mara kwa mara, tangu Januari 8 mwaka jana kila nilipomsikia Edward Lowassa akitajwa.  Januari 8, 2018, ndiyo siku Lowassa alipopokewa rasmi Ikulu na Rais John Pombe Magufuli. Baadaye Lowassa alisema alifurahishwa mno na mkutano wao, kwamba walizungumza mengi na alimpongeza Rais “kwa kazi nzuri anayofanya”.  Mkutano huo baina ya Rais ambaye pia ni mwenyekiti… Continue reading JPM ameshinda walau kwa sasa

MCHAMBUZI MAALUM, SIASA

Nyerere hakuwa na insafu juu ya Muungano

MARA ya mwanzo kabisa kukutana na Mwalimu Julius Nyerere, uso na macho, ilikuwa 1968 jijini London ndani ya ukumbi mmoja wa hoteli iitwayo Hyde Park Hotel.  Hoteli hiyo iko mkabala wa uwanja wa Hyde Park na iko mwendo wa dakika chache kutoka Hertford Street ulipokuwako siku hizo ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza. Sikumbuki iwapo Nyerere alikuwa… Continue reading Nyerere hakuwa na insafu juu ya Muungano