HABARI

Wazanzibari 40,000 waushitaki Muungano

Jumla ya Wazanzibari 40,000 wamesaini waraka wa kumshitaki Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar pamoja na mamlaka nyengine, wakipinga uhalali wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa madai ya kutokuwa na maslahi kwa upande wa Zanzibar. Kesi yao imewasilishwa kwenye Mahakama ya Afrika Mashariki na imepangiwa kusikilizwa mapema mwezi Machi 2018. Msikilize hapa kiongozi wa Wazanzibari hao,… Continue reading Wazanzibari 40,000 waushitaki Muungano

HABARI

Wapi neno mwanana hutumika?

Mtu mwanana, mti mwanana, upepo mwanana, LAKINI Kiswahili chanana, nyumba nyanana. Mzizi wa sifa hii ni -anana. Kwa hivyo, inahitaji kiambishi awali cha jina la kitu kinachopawa sifa. Najua kwamba kuna wengi watumiao "mwanana" kwa kila ngeli. Kwa maoni yangu, hicho si Kiswahili fasaha. Nilipokuwa mdogo, nilikuwa nikiwasikia wazee wakiitumia sifa hiyo, -anana, kwa vitu… Continue reading Wapi neno mwanana hutumika?

HABARI

Juza, juvya, na julisha

Neno "juvya" si 'athari ya matamshi tu' bali ni mbadala wa "juza" na "julisha." Liko katika lahaja ya Kimvita ( na latumika mpaka hivi leo), na nafikiri  liko katika Kipemba na Kimtang'ata pia. Kabla ya hizi harufu (herufi) za Kilatini kutumika mwishoni mwa karne ya 19 kuandikia Kiswahili, lugha hii ilikuwa ikiandikwa kwa harufu za… Continue reading Juza, juvya, na julisha

HABARI

Ni “tanzia” au “taazia”?

Chembelecho (au chambilecho, au chambacho) msemo wa Kiswahili, "Kipya kinyemi, kingawa kidonda." Ni dasturi ya baadhi ya watu kuvutiwa na kipya kitokacho kwengine, hata kama tangu hapo wanacho chao wenyewe kifananacho na hicho cha kigeni. Hili swala la maneno kama "mubashara" lina tanzu mbili. Utanzu wa kwanza ni huo wa kupenda kukimbilia maneno  ya kigeni,… Continue reading Ni “tanzia” au “taazia”?

HABARI

Ni “kiasi cha…” sio “kiasi ya…”

Kwa uchache wa nifahamuvyo, lugha fasaha ni kusema "kiasi cha...", basi haidhuru iwe ni kwa watu au kwa vitu. Yaani, kiasi cha watu kumi, au kiasi cha miti kumi. Kama  ambavyo twasema, kitabu cha..., kisa cha..., kiatu cha..., kitambo cha..., na kadhalika, wala hatusemi kitabu ya..., kisa ya..., kiatu ya..., wala kitambo ya... Na ni… Continue reading Ni “kiasi cha…” sio “kiasi ya…”