MCHAMBUZI MAALUM

Muungano unalindwa kwa nguvu

RAIS Ahmed Abdallah wa Comoro aliyeuliwa Novemba 26, 1989 na askari wa kizungu aliowakodi mwenyewe, anakumbukwa kwa mengi.  Kuna wanaomuona kuwa shujaa kwa kuthubutu kuikabili Ufaransa na kutangaza kuwa Comoro ni taifa huru Julai 6, 1975. Wapo pia wanaomlaumu kwa kuwa sababu ya kumeguka kwa kisiwa chane cha Mayotte ambacho hadi leo kimo mikononi mwa Ufaransa.… Continue reading Muungano unalindwa kwa nguvu

HABARI

Jinsi tawala za kifamilia zinavyouwa demokrasia Afrika

Zipo sababu nyingi zilizomfanya Robert Mugabe ashinikizwe na jeshi na kisha chama chake kujiuzulu. Lakini sababu kubwa na ambayo chama chake ZANU-PF na hata Bunge, kiliiweka mbele ni suala la kuimiliki Zimbabwe kama mojawapo ya mali zake za kifamilia. Bunge lilisema lingemwondoa Rais Mugabe kwasababu mkewe Grace Mugabe amenyang’anya (usurp) madaraka ya urais wakati yeye… Continue reading Jinsi tawala za kifamilia zinavyouwa demokrasia Afrika

HABARI

Kwani upinzani wa kisiasa ni adui wa maendeleo?

ZIMEKUWEPO  hisia miongoni mwa nchi za Kiafrika kuwa upinzani wa kisiasa ni kama njia ya kuzorotesha maendeleo! Hisia hizo zinatolewa na serikali zinazokuwa zimeingia madarakani kwa njia ya kudai demokrasia na baada ya kuukalia usukani zikatamani kuiziba njia hiyo ili isije kutumiwa na wengine, pamoja na serikali zilizodumu madarakani muda wote bila kuonesha maendeleo chanya. Mfano,… Continue reading Kwani upinzani wa kisiasa ni adui wa maendeleo?

HABARI

Labda shetani ndio awape tunzo viongozi wa Afrika

Ni mwaka wa pili sasa kwa Wakfu wa Mo Ibrahim kushindwa kupata mtu wa kumtunuku Tunzo ya Uongozi Bora Afrika. Katika hali ya kushangaza, kamati maalum kwa ajili ya kuteuwa kiongozi wa kumpa tunzo hiyo haijapata kiongozi hata mmoja anayefaa kwenye mataifa 53 ya bara letu hili. Hii ni baada ya kamati hiyo iliyoongozwa na… Continue reading Labda shetani ndio awape tunzo viongozi wa Afrika

HABARI

Uzalendo unaoibuka kwa kufutiwa misaada ni unafiki

Laiti kama haya ya kufutwa kwa awamu ya pili ya msaada wa kimaendeleo wa shirika la misaada la Marekani (MCC) kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yangelitokea kwa Afrika Kusini wakati wa kufinywa kwa demokrasia na ubaguzi, basi tungelipiga makofi. Kama ilivyo kwa Tanzania, hata makaburu walichokuwa nacho wakati ule ni katiba, lakini jee ilitosheleza kusema… Continue reading Uzalendo unaoibuka kwa kufutiwa misaada ni unafiki