SIASA

Chini ya muundo huu wa Muungano, michezo ya Z’bar haisongi mbele – Ally Saleh

Mwanamichezo wa siku nyingi ambaye ni mwanasiasa, mshairi na mwandishi wa habari, Ally Saleh, anasema kuwa muundo wa Muungano uliopo unairejesha nyuma Zanzibar kwenye eneo la michezo, ambalo japokuwa si miongoni mwa mambo ya Muungano, linaikosesha kufaidika na vipaji vyake kimataifa. https://www.youtube.com/watch?v=FiYxSjH2LO8

UTAMADUNI

Mbunge Ally Saleh achapisha diwani nyengine ya ushairi

Mwandishi wa habari aliyesomea sheria na kugeuka kuwa mwanafasihi na kisha mwanasiasa, Ally Saleh (Alberto), amechapisha diwani yake nyengine ya ushairi, inayoitwa 'TUPO: Diwani ya Tungo Twiti', ambayo ni mkusanyiko wa tungo zilizowahi kutumwa kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter. Licha ya kuandikwa kwake kwa lugha ya kifasihi, tungo hizi zina ujumbe mkali wa kisiasa,… Continue reading Mbunge Ally Saleh achapisha diwani nyengine ya ushairi

HABARI

Mbunge wa Malindi amlima barua Infantino wa FIFA

Mbunge wa jimbo la Malindi, mwandishi wa habari na mwanamichezo, Ally Saleh, amemuandikia barua ya wazi Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Gianni Infantino, siku chache kabla ya kiongozi huyo wa soka ulimwenguni kuwasili kwa ziara maalum nchini Tanzania. Kujuwa yaliyomo kwenye barua hiyo, soma hapa. OPEN LETTER Your Excellency Gianni Infantino President FIFA… Continue reading Mbunge wa Malindi amlima barua Infantino wa FIFA

HABARI

Wabunge CUF kwenda mahakamani kuhusu FIFA

Wabunge wanaowakilisha Chama cha Wananchi (CUF) bungeni wanasema kwamba watakwenda mahakamani kusaka majawabu juu ya masuala kadhaa ya michezo, likiwemo la "uhalali wa kikatiba wa Shirikisho la Soka la Tanzania Bara (TFF)" na "tafsiri wa Waziri wa Michezo wa Tanzania Bara kutumika kama ni Waziri wa Muungano ndani ya nchi na nje ya nchi." ┬áZaidi… Continue reading Wabunge CUF kwenda mahakamani kuhusu FIFA

HABARI

Kalamu ya Ally Saleh kwenye ‘La Kuvunda’

Uandishi wa hadithi fupi unafanana na uandishi wa ushairi. Mote muwili, mwandishi hulieleza jambo kubwa na zito kwa maneno machache. Bila ya shaka hadithi fupi ni refu sana kuliko shairi, lakini ni fupi sana kuliko riwaya au hata novela. Mshairi hutafautiana na mwandishi wa hadithi fupi kwenye matumizi ya lugha, mapigo ya sauti na muziki… Continue reading Kalamu ya Ally Saleh kwenye ‘La Kuvunda’