KALAMU YA GHASSANI

Nguvu ya Lissu ni kubwa kuliko ya risasi

Sisi wengine tangu siku ya mwanzo akina Nape Nnauye walipokuwa wakitetea uamuzi wa serikali ya awamu ya tano kuzuia matangazo ya moja kwa moja ya bunge kupitia televisheni ya taifa kwa madai ya kubana matumizi, tulijuwa wameshachelewa. Si katika zama hizi za mawasiliano ya mitandao ya kijamii, ambapo nguvu hasa za mawasiliano zimo viganjani mwa… Continue reading Nguvu ya Lissu ni kubwa kuliko ya risasi

HABARI

Viti maalumu ni kwa ajili ya kuwainua au kuwadidimiza wanawake?

UCHAGUZI  mkuu uliomalizika nchini Kenya umetuachia mengi ya kuyaangalia na kujifunza. Nitajaribu kufananisha machache ambayo yanatuachia mengi ya kujiuliza kwa nini sisi Tanzania yatushinde?   Mara baada ya Rais Kenyatta kutangazwa kuwa ndiye mshindi wa kiti cha urais alisema bila masimango ya aina yoyote kwamba iliyoshinda ni Kenya wala siyo yeye. Wakati Tanzania ilisemwa kwamba… Continue reading Viti maalumu ni kwa ajili ya kuwainua au kuwadidimiza wanawake?

HABARI

Kwa nini siwezi kuuamini muhimili huu katika madini 

Wabunge wa chama fulani na ambao kutokana na wingi wao ndio waamuzi wa kila kitu kwenye muhimili huo uliotakiwa kuwa muhimu nchini petu, nao wanataka tuwaamini na tuliamini bunge hili kwenye hili sakata la madini. Lakini wenye akili wanajiuliza waaminiwe kwa lipi? Ni muhimili huu huu ambao mwaka 1997 ulipitisha kwa dharura sheria mbili: ile… Continue reading Kwa nini siwezi kuuamini muhimili huu katika madini