MCHAMBUZI MAALUM, SIASA

JPM ameshinda walau kwa sasa

“LINI?”  Ni swali nililojiuliza, mara kwa mara, tangu Januari 8 mwaka jana kila nilipomsikia Edward Lowassa akitajwa.  Januari 8, 2018, ndiyo siku Lowassa alipopokewa rasmi Ikulu na Rais John Pombe Magufuli. Baadaye Lowassa alisema alifurahishwa mno na mkutano wao, kwamba walizungumza mengi na alimpongeza Rais “kwa kazi nzuri anayofanya”.  Mkutano huo baina ya Rais ambaye pia ni mwenyekiti… Continue reading JPM ameshinda walau kwa sasa

HABARI

Lema awashukia Nchemba, Kipilimba, Sirro

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA), amewaonya vikali na waziwazi Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba; Mkuu wa Usalama wa Taifa, Modestus Kipilimba; na Mkuu wa Polisi Simon Sirro dhidi ya kile anachosema ni muelekeo wao wa kuipeleka Tanzania kwenye machafuko makubwa ya wenyewe kwa wenyewe.   https://www.youtube.com/watch?v=rrR1QIfFBYg

HABARI

Mbowe na wenzake wafutiwa dhamana, wasubiri kupandishwa kizimbani

Viongozi sita wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), akiwamo Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe wamefutiwa dhamana na kuwekwa mahabusu katika Kituo Kikuu cha Polisi (Central), jijini Dar es Salaam. Pamoja na Mbowe, viongozi wengien ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Vincent Mashinji, Naibu Katibu Mkuu Bara, John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum… Continue reading Mbowe na wenzake wafutiwa dhamana, wasubiri kupandishwa kizimbani

HABARI

Mbowe aitwa tena polisi, atowa waraka mzito kwa taifa

Leo tarehe 22 Machi 2018, mimi na viongozi wenzangu waandamizi wa Chadema tumetakiwa tena kuripoti Polisi. Tunaokabiliwa na usumbufu huu ni pamoja na Mhe Vincent Mashinji (Katibu Mkuu), Mhe. John John Mnyika, Mbunge na Naibu Katibu Mkuu Bara, Mhe. Salum Mwalimu Naibu Katibu Mkuu, Zanzibar; Mhe Halima J. Mdee, Mbunge na Mwenyekiti wa Bawacha, Taifa… Continue reading Mbowe aitwa tena polisi, atowa waraka mzito kwa taifa