HABARI

Mbowe aitwa tena polisi, atowa waraka mzito kwa taifa

Leo tarehe 22 Machi 2018, mimi na viongozi wenzangu waandamizi wa Chadema tumetakiwa tena kuripoti Polisi. Tunaokabiliwa na usumbufu huu ni pamoja na Mhe Vincent Mashinji (Katibu Mkuu), Mhe. John John Mnyika, Mbunge na Naibu Katibu Mkuu Bara, Mhe. Salum Mwalimu Naibu Katibu Mkuu, Zanzibar; Mhe Halima J. Mdee, Mbunge na Mwenyekiti wa Bawacha, Taifa… Continue reading Mbowe aitwa tena polisi, atowa waraka mzito kwa taifa

HABARI

Jinsi tawala za kifamilia zinavyouwa demokrasia Afrika

Zipo sababu nyingi zilizomfanya Robert Mugabe ashinikizwe na jeshi na kisha chama chake kujiuzulu. Lakini sababu kubwa na ambayo chama chake ZANU-PF na hata Bunge, kiliiweka mbele ni suala la kuimiliki Zimbabwe kama mojawapo ya mali zake za kifamilia. Bunge lilisema lingemwondoa Rais Mugabe kwasababu mkewe Grace Mugabe amenyang’anya (usurp) madaraka ya urais wakati yeye… Continue reading Jinsi tawala za kifamilia zinavyouwa demokrasia Afrika

KALAMU YA GHASSANI

Lissu wa dhahabu

Mkononi mwangu nina kitabu kiitwacho 'A Golden Opportunity? Justice & Respect in Mining' (Fursa ya Dhahabu? Haki na Heshima kwenye Madini) cha mwaka 2008. Waandishi wake ni wawili – Mark Curtis na Tundu Lissu. Ni matokeo ya utafiti uliofanywa na wawili hao wakiwa chini ya Baraza la Wakristo Tanzania (CCT) na Baraza la Waislamu Tanzania… Continue reading Lissu wa dhahabu

KALAMU YA GHASSANI

Maisha yasiyotathminiwa hayana maana kuyaishi

Ulimwenguni kote na katika zama zote, jamii inapokuwa chini ya utawala ulioziba masikio na macho na nyoyo, watawala hupenda waachiwe wafanye watakavyo. Huwa wamejirithisha wenyewe nchi na raia wake. Na kwa hili hawataki muhali, masahihisho, wala mabadiliko. Anapotokea mtu kuwasahihisha, badala ya kumchukulia kuwa msaidizi, wao humchukulia adui wao nambari moja, na hivyo hujihalalishia kumuadhibu… Continue reading Maisha yasiyotathminiwa hayana maana kuyaishi

HABARI

Kikwete si wa kuyasema haya

Katika wiki iliyopita, vyombo vya habari nchini Tanzania vilijawa na habari na tahariri kuhusu marais wawili wastaafu wakiwa kwenye jukwaa la viongozi wastaafu wa Afrika nchini Afrika Kusini. Katika mkutano huo, ambao marais Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete walialikwa kujumuika na wastaafu wenzao barani Afrika kuzungumzia mambo yanayoliathiri bara la Afrika, waliripotiwa kuisemea vizuri demokrasia,… Continue reading Kikwete si wa kuyasema haya