UTAMADUNI

Mbunge Ally Saleh achapisha diwani nyengine ya ushairi

Mwandishi wa habari aliyesomea sheria na kugeuka kuwa mwanafasihi na kisha mwanasiasa, Ally Saleh (Alberto), amechapisha diwani yake nyengine ya ushairi, inayoitwa 'TUPO: Diwani ya Tungo Twiti', ambayo ni mkusanyiko wa tungo zilizowahi kutumwa kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter. Licha ya kuandikwa kwake kwa lugha ya kifasihi, tungo hizi zina ujumbe mkali wa kisiasa,… Continue reading Mbunge Ally Saleh achapisha diwani nyengine ya ushairi

UTAMADUNI

‘Kilio cha Usumbufu’: Diwani mpya yaingia sokoni rasmi

Kampuni ya uchapishaji ya mtandaoni, Zanzibar Daima Publishing House, imechapisha diwani mpya ya ushairi wa Kiswahili iitwayo 'Kilio cha Usumbufu' iliyoandikwa na mtaalamu wa lugha na fasihi na mwalimu wa siku nyingi, Maalim Ali Abdulla Ali. Diwani hiyo, ambayo inaanza kuuzwa leo katika mtandao wa Amazon na washirika wake kote ulimwenguni, ina zaidi ya tungo… Continue reading ‘Kilio cha Usumbufu’: Diwani mpya yaingia sokoni rasmi

UTAMADUNI

Kutana na Ally Hilal 3 ndani ya 1

Ingawa kanuni ya maisha inatuelekeza kuwa kila mwanaadamu amezaliwa akiwa na kipaji cha aina fulani, lakini si kila mmoja anayekigunduwa na kukitumia kwa maslahi yake na wengine. Matokeo yake ni kwamba wengi wetu huzaliwa, kukuwa na kufa na vipaji vyetu tukaenda navyo kaburini, bila hata kufahamika kwamba tulikuwa navyo. Havikutufaa wenyewe wala wenzetu. Hivyo sivyo… Continue reading Kutana na Ally Hilal 3 ndani ya 1

HABARI

Riwaya: Safari ya Kumuua Rais – 1

“Hali ya hewa unaiyonaje? , Talib alimuuliza Abdull, huku akimtazama usoni mkononi ameshika chupa ya maji akishushia kooni kukata ukali wa kiu. “Huku kunaonekana ni joto kidogo”, alijibu , macho yake yakipishana na mandhari ya majani ya kijani yanayovutia , kupitia dirisha la kioo cha basi la abiria walillokuwa wanasafiri. “Leo nimemkumbuka sana Fartuun”, kisha… Continue reading Riwaya: Safari ya Kumuua Rais – 1

UTAMADUNI

Machozi Yamenishiya: Diwani ya Mohammed Ghassani

MSHAIRI NA DIWANI YAKE Linapokuja suala la kutaja mafanikio ya mshairi fulani, inatubidi kwanza tulikabili suala gumu la ki-ontolojia: ‘shairi ni nini’? Kwa vile suala hili hukosa jibu mwafaka, mimi hulipa fasili rahisi tu – yaani shairi ni umbo la sanaa-lugha linalojitofautisha na maumbo mengine ya sanaa-lugha kwa jinsi linavyosikika likisomwa kimoyomoyo au kinywa kipana.… Continue reading Machozi Yamenishiya: Diwani ya Mohammed Ghassani