SIASA

Aliyeupeleka Muungano mahakamani ahofia maisha yake

Kiongozi wa vuguvugu la Wazanzibari linalohoji uhalali wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Rashid Salum Adi, ameuomba Umoja wa Mataifa kumpa hifadhi ya usalama wake wakati huu kesi yao ikikaribia kutajwa kwenye Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki mjini Arusha. https://www.youtube.com/watch?v=C0S9tRxWAmU

HABARI

CCM Zanzibar hawana uhalali wa kumshambulia Kabudi

Nikiwa Mzanzibari, Mwanasiasa Mstaafu nimeshangazwa mno na lawama anazotupiwa Prof. Kabudi kutoka kwa Viongozi Waandamizi wa CCM Zanzibar, wakiwemo Wawakilishi na hata Mawaziri kufuatia kauli aliyoitoa Bungeni hivi karibuni kutetea MFUMO wa KATIBA zetu mbili. Sitaki kujadili USAHIHI wa kauli yake, na pia niseme kuwa sikushangazwa na Wazanzibari wasio CCM waliopinga kauli ile ya Prof.… Continue reading CCM Zanzibar hawana uhalali wa kumshambulia Kabudi

KALAMU YA GHASSANI

Serikali inapojibu mabomu ya Lissu kwa risasi za maji

Inaonekana mtazamo wa serikali ya Rais John Magufuli kumuelekea mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), Tundu Lissu, unaanza kubadilika. Kutoka kumkamatakamata kila akitoa kauli na kumweka ndani kisha kumfungulia mashitaka yasiyo kichwa wala miguu, sasa serikali imeamua kujibizana naye neno kwa neno, ‘bandika-bandua’ wasemavyo… Continue reading Serikali inapojibu mabomu ya Lissu kwa risasi za maji

KALAMU YA GHASSANI

Magufuli anawauzia Watanzania tamaa ya maendeleo kwa gharama ya demokrasia yao

Kwa hakika, Rais John Magufuli anaonekana kuwalazimisha raia wake kufanya naye biashara ya gizani. Yeye awauzie maendeleo, nao wamlipe kwa gharama ya demokrasia angalau hadi mwaka 2020 wakati wa kampeni za uchaguzi mwengine. Lakini je, biashara hii inawezekana kwa taifa ambalo lilishaonja ladha ya demokrasia kwa robo karne nzima mtawaliya? Je, ili kupata maendeleo ni… Continue reading Magufuli anawauzia Watanzania tamaa ya maendeleo kwa gharama ya demokrasia yao

MCHAMBUZI MAALUM

Kinachowafanya Uamsho waendelee kusota rumande

Serikali zote duniani zinakuwa na nguvu nyingi, ukiacha vyombo vya dola ambavyo siku zote husimama imara vikiwa upande wao, hata ikitokea serekali inaboronga basi wao huendelea tu kusimama nayo. Ni mara chache sana vyombo vya dola kuwa kinyume na serekali, inatokea lakini ni baada ya mure mrefu wa kuwa bega kwa bega na serekali, hata… Continue reading Kinachowafanya Uamsho waendelee kusota rumande