TAALUMA

Tambua haki zako ukiwa mikononi mwa polisi

Kukamatwa na polisi si kosa, bali ni utaratibu wa kisheria tu. Kwa hivyo, hata unapotiwa nguvuni kwa tuhuma ya kosa fulani, bado wewe hujawa mkosa, na bado una haki zako kamili kama raia na kama mwanaadamu. Kuzijuwa haki hizo, ambatana na Wakili Msomi Omar Said Shaaban akikufahamisha kwa undani zaidi. https://www.youtube.com/watch?v=9cm4pBlvxgU&t=5s

KALAMU YA GHASSANI

Serikali inapojibu mabomu ya Lissu kwa risasi za maji

Inaonekana mtazamo wa serikali ya Rais John Magufuli kumuelekea mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), Tundu Lissu, unaanza kubadilika. Kutoka kumkamatakamata kila akitoa kauli na kumweka ndani kisha kumfungulia mashitaka yasiyo kichwa wala miguu, sasa serikali imeamua kujibizana naye neno kwa neno, ‘bandika-bandua’ wasemavyo… Continue reading Serikali inapojibu mabomu ya Lissu kwa risasi za maji

HABARI

La Lema tayari, sasa la Uamsho

Wanasharia na watetezi wa haki za binaadamu wanatuambia kuwa haki ina misingi yake mikuu, ambayo inapaswa kuhishimiwa ili haki hiyo iitwe kweli ni haki. Mmojawapo ni ukweli kuwa haki na ubinaadamu havitenganishiki. Maana yake ni kuwa viwili hivi ni sawa na kitu kimoja, na ndio maana kinapoondoshwa kimoja, huwa kimeondoshwa chengine. Inapovunjwa haki fulani ya… Continue reading La Lema tayari, sasa la Uamsho