HABARI

Vijana 3 wa Pemba waliotekwa wasimulia mkasa mzima

Vijana watatu kati ya sita waliotekwa kutoka majumbani mwao huko Mtambwe kaskazini mwa kisiwa cha Pemba, wamesimulia mkasa mzima ulivyowatokea tangu walipovamiwa majumbani mwao usiku wa kuamkia Ijumaa (Aprili 6) hadi walipotupwa jana kwenye maeneo ya Ngwachani, kusini mwa kisiwa hicho. https://www.youtube.com/watch?v=X2f6w41H2fc

HABARI

Mazombi wahasiri tena Zanzibar 

Taarifa kutoka kisiwani Unguja zinasema kuwa kwa mara nyengine tena kundi la kiharamia, linalofahamika na wakaazi wa kisiwa hicho kama Mazombi, limemvamia, kumpiga na kumuibia kijana mmoja na kumuwacha mahututi. https://soundcloud.com/mohammed-k-ghassani/mazombi-washambulia-tena Kwa mujibu wa mama wa kijana huyo, Bi Rukia Ali Faki, mwanawe aitwaje Abdullah Ahmeid Juma (miaka 29), mkaazi wa Mchangani, ni mfanya biashara… Continue reading Mazombi wahasiri tena Zanzibar 

HABARI

Mazombi ya Zanzibar ni mfano wa ‘death squads’

Ripoti ya shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International ya mwaka 1975-76 inaseama “vikosi vya usalama vya Argentina vilianza kutumia kile kiitwacho makundi ya mauaji (death squads) mwishoni mwa mwaka 1973. Mfano wa vikosi hivyo ni Alianza Anticomunista Argentina,  ambacho kwa mujibu wa Amnesty International kilisababisha vifo vya takribani watu 1,500, huku… Continue reading Mazombi ya Zanzibar ni mfano wa ‘death squads’

HABARI

CUF yasema sasa imechoka na udhalilishaji

Katika hali isiyo ya kawaida na baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu dhidi ya kile kinachokiita "njama za makusudi dhidi yake", sasa Chama cha Wananchi (CUF) kinasema hakitaweza tena kuvumilia vitendo vya kihuni na kihalifu wanavyotendewa viongozi na wafuasi wake visiwani Zanzibar, kwani wameshasukumwa hadi kwenye ukuta. Akizungumza na wakaazi wa Dunga Kiembeni, wilaya… Continue reading CUF yasema sasa imechoka na udhalilishaji

HABARI

Mazombi wanataka kuizuishia balaa Zanzibar

Katika siku za karibuni, Jeshi la Polisi Zanzibar mara kwa mara limekuwa likitoa tahadhari kwa wananchi kujiepusha na vitendo vinavyoweza kusababisha kuchafuka kwa amani visiwani. Taarifa ya karibuni ya Naibu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai, Salum Msangi, imeeleza kwamba polisi wanawasaka watu wanaodaiwa kuendesha kampeni ya vitisho kwa kuchora alama ya X katika nyumba wanazoziona… Continue reading Mazombi wanataka kuizuishia balaa Zanzibar