UTAMADUNI

Kurasa Mpya: Fungamano la Malenga

Ushairi unatambuliwa kuwa miongoni mwa sanaa kongwe kabisa kwa mwanaadamu. Jamii yoyote inayojitambuwa kwa ukale na ukongwe wake, basi utaikuta ndani yake ikiwa na sanaa ya ushairi kama moja ya dalili za uwepo wake wa zama na zama. Haitoshi hayo, ushairi pia unachukuliwa na wasomi wa taaluma za kibinaadamu, kuwa moja ya nguzo kuu za… Continue reading Kurasa Mpya: Fungamano la Malenga

UTAMADUNI

Kalamu ya Mapinduzi: Mapambano Yanaendelea

Ni jambo gumu kuyazungumzia maandishi bila ya kumgusa mwandishi wake, khasa pale maandishi yenyewe yanapokugusa na kuchoma mithali ya hivi zilivyo tungo za Kalamu ya Mapinduzi na unapokuwa unamfahamu mwandishi binafsi. Nimemjua Mohammed Ghassani kwa zaidi ya miaka kumi kupitia maandishi yake mbalimbali yanayochapishwa kwenye magazeti ya Kiswahili nchini Tanzania. Sehemu kubwa pia ya maandishi… Continue reading Kalamu ya Mapinduzi: Mapambano Yanaendelea

LUGHA, UTAMADUNI

N’na Kwetu: Sauti ya Mgeni Ugenini

Siku ilikuwa Jumatano. Tarehe ilikuwa 1 Septemba 2010. Majira yalikuwa ya saa 4:00 usiku. Mahala palikuwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K. Nyerere jijini Dar es Salaam, mji mkuu wa kibiashara wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Nakumbuka kila kitu kuhusu siku hiyo. Nikiwa kwenye sehemu ya kusafiria abiria waitwao wa kimataifa, nilitoa… Continue reading N’na Kwetu: Sauti ya Mgeni Ugenini

UTAMADUNI

Siwachi Kusema: Uhuru U Kifungoni

Kusema ni moja kati ya njia za kuwasiliana na kuwasiliana kwenyewe ni miongoni mwa tabia za viumbe hai, kwa mujibu wa wataalamu wa mawasiliano. Mtu ambaye hawasiliani, au hana uwezo wa kuwasiliana, huchukuliwa kuwa amekosa kitu muhimu sana kwenye maisha yake, kama vile ambavyo angelichukuliwa mtu asiyeweza kupumua, kutoa uchafu na ama kutembea. Kusema kwenyewe… Continue reading Siwachi Kusema: Uhuru U Kifungoni

UTAMADUNI

Andamo: Sauti ya ushairi kutoka ughaibuni

MIAKA mitano iliyopita nilipata kueleza namna ambavyo wanafunzi wa Chuo cha SOAS (School of Oriental and African Studies) cha nchini Uingereza wanavyofanya juhudi¬† kubwa kujifunza lugha ya Kiswahili. Nilisema lugha ya Kiswahili ni adhimu, katu haitakuja kuachwa nyuma katikati ya utandawazi. Kwamba ni vigumu kwa utandawazi kukifuta au kushusha ari ya kuenea na kujifunza lugha… Continue reading Andamo: Sauti ya ushairi kutoka ughaibuni