MCHAMBUZI MAALUM

Muungano unalindwa kwa nguvu

RAIS Ahmed Abdallah wa Comoro aliyeuliwa Novemba 26, 1989 na askari wa kizungu aliowakodi mwenyewe, anakumbukwa kwa mengi.¬†¬†Kuna wanaomuona kuwa shujaa kwa kuthubutu kuikabili Ufaransa na kutangaza kuwa Comoro ni taifa huru Julai 6, 1975. Wapo pia wanaomlaumu kwa kuwa sababu ya kumeguka kwa kisiwa chane cha Mayotte ambacho hadi leo kimo mikononi mwa Ufaransa.… Continue reading Muungano unalindwa kwa nguvu

MCHAMBUZI MAALUM, SIASA

Nyerere hakuwa na insafu juu ya Muungano

MARA ya mwanzo kabisa kukutana na Mwalimu Julius Nyerere, uso na macho, ilikuwa 1968 jijini London ndani ya ukumbi mmoja wa hoteli iitwayo Hyde Park Hotel.  Hoteli hiyo iko mkabala wa uwanja wa Hyde Park na iko mwendo wa dakika chache kutoka Hertford Street ulipokuwako siku hizo ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza. Sikumbuki iwapo Nyerere alikuwa… Continue reading Nyerere hakuwa na insafu juu ya Muungano

SIASA

Chini ya muundo huu wa Muungano, michezo ya Z’bar haisongi mbele – Ally Saleh

Mwanamichezo wa siku nyingi ambaye ni mwanasiasa, mshairi na mwandishi wa habari, Ally Saleh, anasema kuwa muundo wa Muungano uliopo unairejesha nyuma Zanzibar kwenye eneo la michezo, ambalo japokuwa si miongoni mwa mambo ya Muungano, linaikosesha kufaidika na vipaji vyake kimataifa. https://www.youtube.com/watch?v=FiYxSjH2LO8

SIASA

SMT haiwezi kukubali Akaunti ya Fedha ya Muungano hata siku moja – Juma Duni

Wakati wabunge wa upinzani kutoka Zanzibar wakiendelea kushikilia ulazima wa kuheshimiwa kwa matakwa ya kikatiba ya kuundwa haraka kwa Akaunti ya Pamoja ya Fedha baina ya Tanzania Bara (Tanganyika) na Zanzibar, mtaalamu wa uchumi na fedha na waziri wa zamani kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar, Juma Duni Haji, amesema Serikali ya Jamhuri… Continue reading SMT haiwezi kukubali Akaunti ya Fedha ya Muungano hata siku moja – Juma Duni