KALAMU YA GHASSANI

Kwaheri Maalim Suleiman Shkeli wa Pandani

Mauti ewe mauti, ukija kama hujaja Huwa waja katikati, ya maisha yetu waja Katikati ya wakati, na kati ya zetu haja Na hata tukikutaja, wewe khabari hupati Nimepokea habari ya Kaka yangu, Mzee wangu, Muhisani wangu, Sheikh Sulaiman Al Shukaili, kuitikia wito wa Aitaye akalazimika kuitikwa. Asubuhi hii karudi kwa Mola wake. Allah Ampokee ilhali… Continue reading Kwaheri Maalim Suleiman Shkeli wa Pandani

HABARI

Tuhuma za mateso dhidi ya mayaya Oman, jibu la Mtanzania

Wapendwa waungwana na wapenda ukweli. Siku hizi za karibuni kumekuwako na upotoshwaji mkubwa wa habari za wafanyakazi wa ndani nchini Oman. Jamani waungwana, Waswahili husema kunya anye kuku akinya bata huambiwa kaharisha. Hizo habari za mayaya Oman ni za fitina na uchochezi uliokithiri na hazitamsaidia mtu yoyote, maana sisi ndio wahitaji zaidi wa hizo ajira… Continue reading Tuhuma za mateso dhidi ya mayaya Oman, jibu la Mtanzania

HABARI

Lulu ya Zanzibar: Bi Suad Al Lamki, mwanasheria mstaafu

Bibi Suad Al Lamki, ambaye kwa sasa anaishi Oman, alikuwa jaji wa pili tu mwanamke kwenye Mahakama ya Tanzania baada ya uhuru. Mazungumzo yangu naye, ambayo yapo hapo kwenye vidio hii yanaibua mengi ambayo yumkini yalikuwa hayasemwi kuhusu Zanzibar ya kabla ya Mapinduzi na hata ya baadaye, nafasi ya ilimu na mwanamke kwenye jamii za… Continue reading Lulu ya Zanzibar: Bi Suad Al Lamki, mwanasheria mstaafu

KALAMU YA GHASSANI

Zanzibar ijifunze maana ya mapinduzi kutoka Oman

Kwa makusudi kabisa, wenye satwa ya kutunga sera na mwelekeo wa taifa letu wanataka ionekane kama kwamba uhusiano kati ya Zanzibar na Oman ulianza mwaka 1832 pale Sayyid Said bin Sultan Al-Busaid alipoanzisha utawala wake kisiwani Unguja na kisha kuhamishia rasmi makao yake makuu kutoka Maskat na kuyaleta kisiwani hapo miaka minane baadaye. Wakirudi nyuma… Continue reading Zanzibar ijifunze maana ya mapinduzi kutoka Oman