HABARI

Vijana 3 wa Pemba waliotekwa wasimulia mkasa mzima

Vijana watatu kati ya sita waliotekwa kutoka majumbani mwao huko Mtambwe kaskazini mwa kisiwa cha Pemba, wamesimulia mkasa mzima ulivyowatokea tangu walipovamiwa majumbani mwao usiku wa kuamkia Ijumaa (Aprili 6) hadi walipotupwa jana kwenye maeneo ya Ngwachani, kusini mwa kisiwa hicho. https://www.youtube.com/watch?v=X2f6w41H2fc

HABARI

Maalim Seif auanika usaliti wa Khalifa kwao

Katika kile kinachoibua hisia za Maalim Seif Sharif Hamad kwa kusalitiwa na baadhi ya jamaa zake wa Pemba kwenye mgogoro wa chama chake unaoendelea sasa, Katibu Mkuu huyo wa Chama cha Wananchi (CUF) ametoa kauli kali zaidi kuwahi kutolewa naye hadharani dhidi ya kundi la wanasiasa hao waliomgeuka, hasa Khalifa Suleiman Khalifa, aliyewahi kuwa mbunge… Continue reading Maalim Seif auanika usaliti wa Khalifa kwao

JAMII

RC Kusini Pemba akasirishwa na matokeo ya Kidato IV

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Hemed Suleiman, amesema kufanya vizuri kwa skuli tatu tu kati ya zaidi ya 20 katika mitihani ya Kidato cha Nne 2017 ndani ya mkoa wake ni jambo la aibu na linalopaswa kuchukuliwa hatua kali kulirekebisha ili lisijirejee. Angalia ripoti ya Kauthar Is-haq kutoka kisiwani Pemba. https://www.youtube.com/watch?v=6D76q2z17mw    

Nassor Mazrui
HABARI

CUF yatoa kauli rasmi ziara ya Lipumba kisiwani Pemba

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Nassor Ahmed Mazrui, kimeikanusha vikali barua iliyotolewa na jeshi la polisi mkoa wa kusini Pemba, likidai kupokea barua ya CUF kuridhia kufanyika kwa kongamano kwenye ukumbi wa Makonyo, Chake Chake kisiwani Pemba hapo kesho (Jumamosi, 24 Februari 2018).   Hii hapa chini ndiyo taarifa rasmi ya CUF… Continue reading CUF yatoa kauli rasmi ziara ya Lipumba kisiwani Pemba

SIASA

CUF Pemba wamuonya Lipumba, polisi

Chama cha Wananchi (CUF) kisiwani Pemba kimetoa onyo kali dhidi ya aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho ngazi ya taifa, Prof. Ibrahim Lipumba, kwamba asijaribu kukanyaga kisiwani huko kuendesha kile kinachoitwa "kongamano la vijana" kwenye ukumbi wa Kiwanda cha Makonyo, Chake Chake, siku ya Jumamosi ya tarehe 24 Februari 2018. Chama hicho pia kimelitahadharisha jeshi la… Continue reading CUF Pemba wamuonya Lipumba, polisi