HABARI

Zaima TV yazindua kipindi maalum cha ‘Ajenda ya Zanzibar’

Kuelekea maadhimisho ya miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar hapo Aprili 26, Zaima TV inaanza kurusha kipindi maalum kiitwacho Ajenda ya Zanzibar, ambacho kinaangazia hoja ya Wazanzibari kuelekea Muungano wenyewe. Nini wanachokisimamia? Nini kinachowakera? Lipi ni suluhisho? Yote yanajibiwa kwenye kipindi hiki na Wazanzibari kwa mtazamo wa Kizanzibari. Usikose. https://www.youtube.com/watch?v=99DoFImx2mw

HABARI, SIASA

Adi afafanua kile hasa kilichotokea kesi ya Muungano EACJ

Kiongozi wa Wazanzibari 40,000 waliofungua kesi ya kuhoji uhalali wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwenye Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki (EACJ), Rashid Salum Adi, amefafanua kwa kina kile hasa kilichotokea jana kwenye mahakama hiyo mjini Arusha, wakati kesi yao ilipotajwa kwa mara ya kwanza kabisa kwa kutanguliza ombi la awali ambalo liliondolewa na… Continue reading Adi afafanua kile hasa kilichotokea kesi ya Muungano EACJ

HABARI

Kesi ya kupinga Muungano kuanza kesho Arusha

Mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ) imeanza kusikiliza kesi zilizofunguliwa na watu binafsi pamoja na mashirika mbalimbali dhidi ya nchi wanachama wa jumuiya na zinatarajiwa kuuanza kusikilizwa hadi Machi 29 mwaka huu. Kati ya kesi zinazotarajiwa kuvuta hisia za wengi ni kesi namba 7 ya mwaka 2017 iliyofunguliwa na Rashid Salum Adiy na wenzake 39,999 dhidi… Continue reading Kesi ya kupinga Muungano kuanza kesho Arusha

SIASA

Aliyeupeleka Muungano mahakamani ahofia maisha yake

Kiongozi wa vuguvugu la Wazanzibari linalohoji uhalali wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Rashid Salum Adi, ameuomba Umoja wa Mataifa kumpa hifadhi ya usalama wake wakati huu kesi yao ikikaribia kutajwa kwenye Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki mjini Arusha. https://www.youtube.com/watch?v=C0S9tRxWAmU

Haji Omari Kheri
KALAMU YA GHASSANI

Ramadhani nyengine imepita, dhuluma dhidi ya Uamsho bado yaendelea

Kwa hakika sijui ni kitu gani kilichokuwa kimenifanya niamini kuwa Ramadhani ya mwaka huu isingelimalizika kabla ya viongozi na wafuasi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu ya Zanzibar (Uamsho) wanaoshikiliwa kwa zaidi miaka minne sasa katika magareza ya Tanzania Bara, hawajaachiliwa huru! Ni jambo la kushangaza kuwa bila ya hata kuwa na ushahidi… Continue reading Ramadhani nyengine imepita, dhuluma dhidi ya Uamsho bado yaendelea