MCHAMBUZI MAALUM

Masauni amelewa pombe gani?

Kijijini kwetu alikuwepo mzee mmoja ambaye alikuwa maarufu sana.  Miongoni mwa mambo yaliyompa umaarufu ni jinsi alivyokuwa mweledi katika elimu ya dini ya Kiislamu kiasi cha kuwafundisha baadhi ya aalim wakubwa katika kijiji hicho.  Pamoja na taaluma aliyokuwa nayo, alikuwa mpenzi mkubwa wa pombe.  Kwa ufupi alikuwa mlevi, unaweza kusema wa kupindukia. Katika sikukuu moja… Continue reading Masauni amelewa pombe gani?

MCHAMBUZI MAALUM

Algeria: Darasa za bure barabarani

KATIKA maktaba yangu nina kitabu, kijitabu kwa hakika, chenye kufundisha namna ya kufanya mashambulizi ya kigaidi katika miji kwa lengo la kupindua serikali. Kinaitwa “Minimanual of the Urban Guerilla” na kimeandikwa na Carlos Marighella, mwanasiasa na mpiganaji wa vita vya mwituni wa Brazil aliyefariki Novemba 1969. Marighella alikuwa mfuasi wa itikadi ya Kimarx na Kilenin.… Continue reading Algeria: Darasa za bure barabarani

MCHAMBUZI MAALUM, SIASA

Maalim Seif na Jahazi la Nuh

Kinachoendelea hivi sasa katika siasa za Tanzania, kwa ujumla, hasa kwa upande wa Zanzibar katika Chama Cha Wananchi (CUF) kimenifanya nikumbuke tarekhe za visa vya Mitume na kwa muktadha wa makala hii fupi nitaangalia kazi kubwa ya kiutume iliyofanywa na Nabii Nuh (AS), upinzani aliokumbana nao na mwisho kulitazama Jahazi la Uokozi aililolichonga kwa amri… Continue reading Maalim Seif na Jahazi la Nuh

MCHAMBUZI MAALUM, SIASA

JPM ameshinda walau kwa sasa

“LINI?”  Ni swali nililojiuliza, mara kwa mara, tangu Januari 8 mwaka jana kila nilipomsikia Edward Lowassa akitajwa.  Januari 8, 2018, ndiyo siku Lowassa alipopokewa rasmi Ikulu na Rais John Pombe Magufuli. Baadaye Lowassa alisema alifurahishwa mno na mkutano wao, kwamba walizungumza mengi na alimpongeza Rais “kwa kazi nzuri anayofanya”.  Mkutano huo baina ya Rais ambaye pia ni mwenyekiti… Continue reading JPM ameshinda walau kwa sasa