MCHAMBUZI MAALUM

Masauni amelewa pombe gani?

Kijijini kwetu alikuwepo mzee mmoja ambaye alikuwa maarufu sana.  Miongoni mwa mambo yaliyompa umaarufu ni jinsi alivyokuwa mweledi katika elimu ya dini ya Kiislamu kiasi cha kuwafundisha baadhi ya aalim wakubwa katika kijiji hicho.  Pamoja na taaluma aliyokuwa nayo, alikuwa mpenzi mkubwa wa pombe.  Kwa ufupi alikuwa mlevi, unaweza kusema wa kupindukia. Katika sikukuu moja… Continue reading Masauni amelewa pombe gani?

HABARI

Viongozi 5 wa Uamsho ‘waachiliwa’

Viongozi watano wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar waliokuwa wametoweka kwenye mazingira ya kutatanisha zaidi ya wiki tatu sasa, wameachiliwa na kurejea majumbani kwao katika mazingira pia ya kutatanisha. Mmoja wa viongozi hao, Amir Haji Khamis, akizungumza kwa hali ya huzuni na wasiwasi, ameiambia Zaima Media hivi leo kwamba hawawezi kuzungumzia zaidi… Continue reading Viongozi 5 wa Uamsho ‘waachiliwa’

HABARI

Viongozi 5 wa Uamsho watoweka kiutatanishi

Viongozi watano wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu visiwani Zanzibar hawajuilikani walipo baada ya kutoweka majumbani mwao kwa takribani wiki ya pili sasa. Miongoni mwao ni Amiri wa Jumuiya hiyo, Hajj Khamis Hajj, ambaye alikuwa kinara wa kukusanya michango kwa ajili ya familia za viongozi wenzao ambao tayari wamekuwako ndani tangu mwaka 2013.… Continue reading Viongozi 5 wa Uamsho watoweka kiutatanishi

MCHAMBUZI MAALUM

Kinachowafanya Uamsho waendelee kusota rumande

Serikali zote duniani zinakuwa na nguvu nyingi, ukiacha vyombo vya dola ambavyo siku zote husimama imara vikiwa upande wao, hata ikitokea serekali inaboronga basi wao huendelea tu kusimama nayo. Ni mara chache sana vyombo vya dola kuwa kinyume na serekali, inatokea lakini ni baada ya mure mrefu wa kuwa bega kwa bega na serekali, hata… Continue reading Kinachowafanya Uamsho waendelee kusota rumande

MCHAMBUZI MAALUM

Guantanamo isifananishwe Segerea

SI sahihi sana kumuingiza Rais John Magufuli katika chungu kimoja tu cha kuukosoa utendaji wake wote. Yapo ambayo anapatia, na kwa nionavyo, kwa hayo, amekuwa mfano kwa viongozi wengine. Mapambano yake dhidi ya ufisadi, ni mfano, ingawa kiutekelezaji zipo kasoro hizi ni na zile. Kuonesha jinsi gani yapo mazuri, wakati mwengine husababisha aibu na fedheha… Continue reading Guantanamo isifananishwe Segerea