UTAMADUNI

Mbunge Ally Saleh achapisha diwani nyengine ya ushairi

Mwandishi wa habari aliyesomea sheria na kugeuka kuwa mwanafasihi na kisha mwanasiasa, Ally Saleh (Alberto), amechapisha diwani yake nyengine ya ushairi, inayoitwa 'TUPO: Diwani ya Tungo Twiti', ambayo ni mkusanyiko wa tungo zilizowahi kutumwa kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter. Licha ya kuandikwa kwake kwa lugha ya kifasihi, tungo hizi zina ujumbe mkali wa kisiasa,… Continue reading Mbunge Ally Saleh achapisha diwani nyengine ya ushairi

UTAMADUNI

Machozi Yamenishiya: Diwani ya Mohammed Ghassani

MSHAIRI NA DIWANI YAKE Linapokuja suala la kutaja mafanikio ya mshairi fulani, inatubidi kwanza tulikabili suala gumu la ki-ontolojia: ‘shairi ni nini’? Kwa vile suala hili hukosa jibu mwafaka, mimi hulipa fasili rahisi tu – yaani shairi ni umbo la sanaa-lugha linalojitofautisha na maumbo mengine ya sanaa-lugha kwa jinsi linavyosikika likisomwa kimoyomoyo au kinywa kipana.… Continue reading Machozi Yamenishiya: Diwani ya Mohammed Ghassani

UTAMADUNI

Siwachi Kusema: Uhuru U Kifungoni

Kusema ni moja kati ya njia za kuwasiliana na kuwasiliana kwenyewe ni miongoni mwa tabia za viumbe hai, kwa mujibu wa wataalamu wa mawasiliano. Mtu ambaye hawasiliani, au hana uwezo wa kuwasiliana, huchukuliwa kuwa amekosa kitu muhimu sana kwenye maisha yake, kama vile ambavyo angelichukuliwa mtu asiyeweza kupumua, kutoa uchafu na ama kutembea. Kusema kwenyewe… Continue reading Siwachi Kusema: Uhuru U Kifungoni

UTAMADUNI

Andamo: Sauti ya ushairi kutoka ughaibuni

MIAKA mitano iliyopita nilipata kueleza namna ambavyo wanafunzi wa Chuo cha SOAS (School of Oriental and African Studies) cha nchini Uingereza wanavyofanya juhudi  kubwa kujifunza lugha ya Kiswahili. Nilisema lugha ya Kiswahili ni adhimu, katu haitakuja kuachwa nyuma katikati ya utandawazi. Kwamba ni vigumu kwa utandawazi kukifuta au kushusha ari ya kuenea na kujifunza lugha… Continue reading Andamo: Sauti ya ushairi kutoka ughaibuni

HABARI

‘Mgogoro’ katika ushairi wa Kiswahili

Mgogoro" katika ushairi wa Kiswahili umekuwapo kwa zaidi ya miaka kumi sasa. Una misingi yake katika utata wa mambo mawili: (i) Maana ya jumla ya shairi (ii) Maana ya shairi la Kiswahili. Mvutano huu, sawa na uk tulioutaja katika nchi za Ufaransa, Uingereza na Marekani, una pande kuu mbili. Upande mmoja wapo wanamapokeo ambao wanasisitiza… Continue reading ‘Mgogoro’ katika ushairi wa Kiswahili